Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanatoa pole mbele ya malalo yake tukufu katika kumbukumbu ya kifo cha Mtume (s.a.w.w)…

Maoni katika picha
Kawaida ya watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kila siku ya Jumanne na Alkhamisi saa nane Aduhuri hufanya ibada maalumu, husimama kwa mistari wakiwa wameelekea katika kaburi tukufu la mwezi wa familia na kusoma ziara kwa pamoja kisha huimba kaswida ya (Ibaa) na humaliza kwa kusoma dua au shairi la Husseiniyya, lakini kuna siku zenye matukio mahsusi, kama vile tarehe za kuzaliwa na kufariki kwa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s), kwa kua bado tupo katika siku za huzuni ya kifo cha Mtume (s.a.w.w) ambaye tarehe ya kifo chake imesadifu siku ya jana Jumatano (28 Safar).

Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) walipo maliza kusoma ziara huku wakiwa wameelekea katika kaburi lake tukufu na kuimba kaswida ya Ibaa, waliimba kaswida za kuomboleza msiba huu mkubwa katika umma wa kiislamu na Ahlulbait (a.s), na kumpa pole mtoto wa ndugu yake na wasii wake kutokana na tukio hili chungu.

Idadi kubwa ya watu wanaokuja kuzuru malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ilishiriki pamoja nao katika maombolezo hayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: