Ofisi ya Marjaa Dini mkuu Ayatullahi Sayyid Ali Husseini Sistani yatangaza kua Ijumaa ya kesho (9 Novomba 2018m) ni siku ya kwanza ya mwezi wa Rabiul Awwal (1440h).
Yamesemwa hayo katika taarifa iliyo tolewa na ofisi ya Mheshimiwa Sayyid Sistani, isemayo kua ofisi ya Mheshimiwa imethibitisha kuandama kwa mwezi wa Rabiul Awwal – 1440h.
Kufuatia tangazo hilo, baada ya swala za Magharibi na Isha za leo (29 Safar 1440h) sawa na (8 Novemba 2018m) bendera za kubba mbili ya Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) zimebadilishwa, zimetolewa za rangi nyeusi na kuwekwa za rangi nyekundu, ikiwa kama alama ya kumaliza kipindi cha huzuni za watu wa nyuma ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) kilicho dumu miezi miliwi, mwezi wa Muharam na Safar.