Hivi ndio hufanya wanachuoni wanapo tembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)…

Maoni katika picha
Imekuja katika athari za ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) iliyo pokewa katika mazaru kubwa ya Ibun Mash-hadi, kwa sanadi sahihi kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s), miongoni mwa adabu zake; Zaairu alishike kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) na alibusu, huku anasema.. (kadha na kadha).

Imekuja katika mazaru ya Shekh Mufiid, na mazaru ya Sayyid Ibun Twausi, wakati Zaairu anapoomba idhini ya kuingia kwenye Raudha tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), aingie na ashike kaburi kisha aseme maneno haya akiwa ameelekea Kibla: (Amani iwe juu yako ewe mja mwema…).

Katika ziara nyingine imeandikwa kua: (kisha utashika kaburi lake tukufu na kusema: Kwa baba, wewe na mama ewe uliye nusuru Dini ya Allah…).

Kwa ajili hiyo wanachuoni wakubwa na Maraajii wanapo kwenda kumzuru Abulfadhil Abbasi (a.s), wanapo ingia katika Raudha yake tukufu, hubusu Ataba yake kama wanavyo busu Ataba ya Imamu Hussein (a.s) kwa utukufu wa kumzuru.

Imepokewa kutoka kwa Allamah Darbandi mwandishi wa kitabu cha (Asraaru Shahada) kua siku moja alimwambia Shekh Answariy, katika siku za Marjaiyya yake: Hakika shia wanakufuateni na kuiga vitendo vyenu, wakati mnapo kwenda kumzuru Imamu Hussein (a.s) lau kama mngekua mnabusu Ataba yake tukufu pale mnapo ingia katika Raudha yake, ili shia wakuigeni katika hilo, wafanye kama mtakavyo fanya ili nanyi mpate thawabu pamoja nao. Shekh Answari akamjibu kua: Mimi hubusu Ataba tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), vipi nisibusu Ataba za Maimamu watoharifu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w) kama Imamu Hussein (a.s).

Kisha akaongeza kua: Hakika mimi nabusu Ataba ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuikumbatia; kwa sababu ndio kimbilio la mazuwaru watukufu, hakika yeye ni mlango wa haja na ndio mlango wa Imamu Hussein (a.s) Abulfadhil Abbasi Ibun Amirul Mu-uminina (a.s).

Hii ni sehemu ya utukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s), anaheshima kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu na Mtume wake (s.a.w.w) na mbele ya mtoto wake Fatuma Zaharaa (a.s), na mbele ya Maimamu watoharifu (a.s) wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), na mbele ya mama yake Ummul Banina (a.s), na mbele ya dada yake bibi Zainabu (a.s), na mbele ya shia wake na wapenzi wake.

Kuhusu ukweli wa heshima ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na uhalisia wa cheo chake hakuna anayejua ispokua Mwenyezi Mungu mtukufu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu aturuzuku kumtembelea na atufufue pamoja naye Duniani na Akhera, Aamina Rabbal-Aalamiina.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: