Baada ya kumaliza ziara ya Arubaini tukufu, miongoni mwa kazi zinazo fanywa na kitengo cha usimamizi wa waharam ya Atabatu Abbasiyya tukufu na kama sehemu ya usimamizi wa kutandika miswala mipya, kazi ya kusafisha haram na uwanja wake mtukufu imekamilika.
Kiongozi wa idara ya haram Ustadh Zainul-Aabidina Adnani ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram siku ya jana wamemaliza kazi ya kuosha haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na huo ndio utaratibu wa kitengo hicho baada ya ziara ya Arubaini, hakika haram hii tukufu ilishuhudia mafuriko ya watu katika ziara ya Arubaini ambayo kila mwaka baada ya ziara hiyo hufanywa kazi ya kuoshwa na kwa ajili ya kulinda usafi wa marumaru na kurekebisha sehemu zilizo haribika”.
Akaongeza kua: “Kazi ya usafi imehusisha upuliziaji wa uturi na kutandika miswala mipya, kazi hizo zimekua zikifanywa usiku wa manane kwa sababu ya uchache wa mazuwaru katika mida hiyo na urahiri wa utendaji”.
Tunapenda kufahamisha kua kazi ya usafi hufanywa kila siku ndani ya mwaka mzima, kwa ajili ya kulinda utukufu na usafi wa eneo hili takatifu na kuhakikisha marumaru na madini yaliyopo katika kaburi hayaharibiki.