Matawi ya Atabatu Abbasiyya tukufu yanafanya maandalizi ya mwisho ya kushiriki katika maonyesho ya kimataifa ya Bagdad…

Maoni katika picha
Maonyesho ya kimataifa ya Bagdad hupewa umuhimu mkubwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, awamu ya (45) ya maonyesho hayo inatarajiwa kuanza siku ya Jumamosi ya kesho chini ya kauli mbiu isemayo: (Tumeazimia kujenga taifa kama tulivyo likomboa na kuleta ushindi) katika uwanja wa maonyesho ya kimataifa mjini Bagdad, ni nisehemu ya muendelezo wa ushiriki wake katika maonyesho yaliyo pita.

Atabatu Abbasiyya tukufu itashiriki maonyesho hayo kupitia matawi nane ikiwa ni pamoja na viwanda mbalimbali, ambayo ni:

  • 1- Vitalu vya Alkafeel: vitaonyesha mimea inayo limwa pamoja na asali.
  • 2- Shirika la Nurul Kafeel linalo tengeneza bidhaa za viumbe hai: litaonyesha bidhaa linazo tengeneza.
  • 3- Shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud: litaonyesha bidhaa linazo tengeneza na namna linavyo pambana na athari za tabia nchi.
  • 4- Shirika la ujenzi la kimataifa Alliwaau linalo jihusisha na viwanda, biahara na uchumi: litaonyesha bidhaa linazo tengeneza ikiwa ni pamoja na (tofali za blok) za aina mbalimbali.
  • 5- Darul Kafeel ya uchapishaji na usambazaji: itaonyesha baadhi ya machapisho yake na vifaa inavyo tumia.
  • 6- Shirika kuu la kiuchumi Alkafeel ambalo lipo chini ya kitengo cha kilimo na ufugaji: litaonyesha mazao yanayo limwa katika mashamba ya Khairaat Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na kuonyesha video za mashamba ya kilimo cha kumwagilia, na mashamba ya Anwaaru Saaqi na Qaadhi Hajaat.
  • 7- Shirika la ulinzi na mawasiliano Alkafeel: litaonyesha huduma linazo toa.
  • 8- Hospitali ya rufaa Alkafeel: itaonyesha huduma mbalimbali inazo toa kwa wananchi.

Wakuu wa matawi yatakayo shiriki, wamesisitiza kua ushiriki wao utakua mzuri kutokana na namna walivyo jiandaa, sambamba na kutambulisha maeneleo yaliyo patikana katika kila sekta.

Kituo cha uchapishaji wa namba Alkafeel kilicho chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimechukua jukumu la kuandaa mabango maalumu ya kila kitengo yanayo endana na vitu vinavyo onyeshwa na kitengo husika.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imekwisha shiriki mara nyingi katika maonyesho ya kimataifa ya Bagdad ambayo huyachukulia kuwa maonyesho muhimu kwake, aidha imeshiriki katika maonyesho mbalimbali ya kimataifa na kitaifa nje na ndani ya Iraq, ambayo husaidia kuonyesha mafanikio yanayo patikana katika vitengo vyake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: