Miongoni mwa mfululizo wa vitabu vinavyo tolewa na kituo cha maarifa ya Qur’ani kuifasiri na kuichapisha kilicho chini ya Maahadi ya Qur’ani tukufu ya Atabatu Abbasiyya vinavyo lenga kufundisha usomaji wa kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa utaratibu mpya na mzuri, kimetoa kitabu kipya kiitwacho (jifunze hukumu za usomaji kwa waanzao) kitabau hiki kimeandikwa baada ya kitabu cha kwanza kiitwacho (jifunze kiarabu kutoka ndani ya Qur’ani tukufu).
Ndani ya kitabu hiki zimeandikwa aya zenye hukumu muhimu kwa ajili ya kusomesha usomaji sahihi kwa wale wanaoanza hatua ya kwanza, na kuhakikisha wanasoma vizuri na wanatamka sahihi bila kukosea hata katika sehemu ambazo watu wengi hukosea, jambo hilo hufikiwa kwa kujifunza hukumu kwa umakini na kwa njia rahisi, hakika watu wengi wanaoishi katika nchi zisizo zungumza kiarabu wanahitaji mfumo mzuri utakao wawezesha kusoma kwa urahisi na haraka.
Ndio sababu kubwa ya kuandikwa kwa kitabu hiki katika mfululizo huu wa vitabu vya (jifunze kutoka ndani ya Qur’ani tukufu), vitabu hivi vinalenga kuwasomesha usomaji wa Qur’ani tukufu watu wasio ongea kiarabu pamoja na kuwafundisha matamshi sahihi ya herufi za kiarabu.
Kumbuka kua kituo cha maarifa ya Qur’ani kuifasiri na kuichapisha ni moja ya vituo muhimu katika Maahadi ya Qur’ani tukufu, kinatekeleza miradi mingi ya Qur’ani tukufu inayo saidia kufundisha utamaduni ya Qur’ani, miongoni mwa miradi hiyo ni uchapishaji wa msahafu wa toleo maalumu la Atabatu Abbasiyya, ambalo ni fanikio kubwa, kwa sababu hii ni mara ya kwanza kuandikwa na kuchapishwa Qur’ani hapa Iraq, wakati misahafu yote ilikua inachapishwa na taasisi za Qur’ani nje ya nchi.