Atabatu Abbasiyya yazindua maonyesho katika matawi yake kwenye maonyesho ya kimataifa ya Bagdad na yatumia kauli mbiu isemayo (Miradi yetu yashajihisha Iraq kujitegemea)…

Maoni katika picha
Katika ushiriki mkubwa wa Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia mashirika, viwanda, kilimo na biashara, Asubuhi ya Jumamosi (2 Rabiul Awwal 1440h) sawa na (10 Novemba 2018m) yamefunguliwa rasmi maonyesho ya kimataifa ya Bagdad chini ya kauli mbiu isemayo: (Tumekusudia kujenga kama tulivyo komboa na kushinda) ambayo yatadumu kwa muda wa siku kumi.

Matawi ya Atabatu Abbasiyya tukufu yamechukua moja ya kauli za kiongozi mkuu wa kiseria na kuifanya kua kauli mbiu, ambayo inasema: (Miradi yetu inashajihisha Iraq kujitegemea), wanaonyesha bidhaa za aina tofauti. Mjumbe wa kamati kuu ya uongozi wa Atabatu Abbasiyya Muhandisi Jafari Saidi Jafari aliyekuwepo wakati wa uzinduzi wa maonyesho hayo ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyesho haya unasaidia kuonyesha bidhaa zinazo tengenezwa na vitengo vyake pamoja na kutambulisha mambo yanayo fanywa na vitengo vyake miongoni mwa juhudi mbalimbali za kujitegemea katika sekta ya viwanda, kilimo na uzalishaji wa chakula, sambamba na kuangalia bidhaa zinazo tengenezwa na mashirika mengine yanayo shiriki katika maonyesho, pia hii ni fursa ya kukutana na mashirika makubwa yanayo shiriki kayika maonyesho hayo”.

Akaongeza kua: “Maonyesho ya Bagdad ni miongoni mwa maonyesho makubwa na muhimu, huanza mapema maandalizi ya kushiriki kwenye maonyesho haya. Ikiwa ni pamoja na awamu hii ya maonyesho ambayo tunatarajia kuendelea kufanya vizuri kama tulivyo fanya katika maonyesho yaliyo pita, tunasisitiza kua Iraq inaviwanda bora, Iraq ni nchi ya viwanda, uwezo na uzowefu wa watu wa Iraq ukitengenezewa mazingira mazuri unaweza kuleta mafanikio makubwa, na hivi ndio tunavyo fanya katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kila tunacho onyesha ni kazi ya mikono yetu”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inashiriki katika maonyesho haya kupitia matawi nane vikiwemo vitengo vya viwanda ambavyo ni:

  • 1- Vitalu vya Alkafeel: vitaonyesha mimea inayo limwa pamoja na asali.
  • 2- Shirika la Nurul Kafeel linalo tengeneza bidhaa za viumbe hai: litaonyesha bidhaa linazo tengeneza.
  • 3- Shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud: litaonyesha bidhaa linazo tengeneza na namna linavyo pambana na athari za tabia nchi.
  • 4- Shirika la ujenzi la kimataifa Alliwaau linalo jihusisha na viwanda, biahara na uchumi: litaonyesha bidhaa linazo tengeneza ikiwa ni pamoja na (tofali za blok) za aina mbalimbali.
  • 5- Darul Kafeel ya uchapishaji na usambazaji: itaonyesha baadhi ya machapisho yake na vifaa inavyo tumia.
  • 6- Shirika kuu la kiuchumi Alkafeel ambalo lipo chini ya kitengo cha kilimo na ufugaji: litaonyesha mazao yanayo limwa katika mashamba ya Khairaat Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na kuonyesha video za mashamba ya kilimo cha kumwagilia, na mashamba ya Anwaaru Saaqi na Qaadhi Hajaat.
  • 7- Shirika la ulinzi na mawasiliano Alkafeel: litaonyesha huduma linazo toa.
  • 8- Hospitali ya rufaa Alkafeel: itaonyesha huduma mbalimbali inazo toa kwa wananchi.

Kituo cha uchapishaji wa namba Alkafeel kilicho chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimechukua jukumu la kuandaa mabango maalumu ya kila kitengo yanayo endana na vitu vinavyo onyeshwa na kitengo husika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: