Mpiga picha wa Atabatu Abbasiyya tukufu apata tuzo tatu katika mashindano ya upigaji picha ya kimataifa, na serikali ya Urusi yamkaribisha mtoto Qassim ambaye yupo katika maudhui ya picha…

Maoni katika picha
Mpiga picha mwenye uwezo mkubwa na ujuzi wa hali yajuu katika kupiga picha amesha pata tuzo za kitaifa na kiarabu, hakutosheka na hapo, bali amekwenda kushiriki katika mashindano ya kimataifa, amepambana na wapiga picha nguli (walio bobea) wa kimataifa na kafanikiwa kupata tuzo kadhaa. Katika shindano la Andereyya huko Urusi la kimataifa amepata tuzo tatu muhimu, naye ni bwana Taisiri Mahdi mmoja wa wapiga picha wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, ushindi huu ni mwenyelezo wa ushindi kama huu aliopata katika mashindano ya kitaifa na kimataifa.

Mpiga picha huyo bwana Taisiri Mahdi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Nimesha shiriki mashindano mengi na asilimia kubwa nilipata nafasi za juu, lakini mashindano haya yalikua tofauti kutokana na wingi wa washiriki wenye uwezo mkubwa na utaalamu wa hali ya juu, lakini hilo halikunizuia kushiriki wala halikunifanya nisitowe ushindani, jumla ya kazi zilizo shiriki zilikua (6,000) wapiga picha walio shiriki wametoka nchi (77), kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu na baraka za tunaye mtumikia nimefanikiwa kupata tuzo tatu, tuzo ya kwanza nimepewa na uongozi wa mashindano ya Andereyya kutokana na picha iliyo kua na maudhui ya kupenda maisha, tuzo ya pili nimepewa na uongozi wa luninga ya Almayaadeen, uliokua unasimamia mashindano na baada ya kuzirusha na kufanya uchambuzi wa picha zinazo endana na kauli mbiu yao isemayo: (Tupo na mwanaadamu kila mahala), na tuzo ya tatu nimepewa na wanahabari wa Shanhai kutoka China”.

Akaongeza kua: “Tuzo kubwa niliyo pewa inatokana na picha zenye ujumbe wa sauti ambao ni wito wa mtoto Qassim kwa serikali ya Urusi, mtoto huyo alivunjika mguu baada ya kushambuliwa na magaidi wakati anacheza mpira wa miguu pamoja na rafiki zake”.

Akabainisha kua: “Irar iling’aa katika ufunguzi wa maonyesho, kila mtu aliizungumzia, tumefanikiwa kufikisha ujumbe duniani kua Iraq kupitia vijana na watoto wake pamoja na mazingira magumu waliyo pitia lakini bado wanaendeleza upendo na kuishi kwa amani, jambo hili liliwashughulisha sana washiriki wa kongamano, kila mtu alipongeza ikiwa ni pamoja na viongozi wakuu wa vyombo vya habari”.

Mzungumzaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi Mariya Zakharufa amesema wako tayali kumkaribisha mtoto wa kiiraq Qassim aliye pigwa picha na bwana Taisiri Mahdi, akabainisha kua: “Tumevutiwa sana na mazingira ya kuonyesha mwanaadamu pamoja na matatizo yake, na uwezo wa kupiga picha zinazo onyesha namna kheri inavyo shinda shari, na ushindi ni matashi, nguvu na ushujaa, hili ni muhimu sana tunapo ongea kuhusu watoto”. Akaendelea kusema kua: “Pindi mtoto anapo nusurika na akapigwa picha maridadi kama za bwana Taisiri Mahdi zinatushajihisha kumkaribisha mtoto huyo hapa Urusi kwa ajili ya matibabu na kumsaidia mambo mengine, ikiwa ni pamoja na kwenda kutembelea uwanja wa mpira wa miguu”.

Kumbuka kua mashindano ya Andereyya ya kimataifa ya wapiga picha wa vyombo vya habari, yameratibiwa na mamlaka ya vyombo vya habari vya kimataifa (Urusi Singhudunya) chini ya uangalizi wa kamati ya taifa la Urusi ya Unesco, mashindano haya, yanakusudia kuwatia moya wapigapicha vijana na kuwafanya watu wajali upigaji picha wa kisasa, waliandaa chopo la majaji ambalo lilimuhusisha mwakilishi wa habari za kimataifa pamoja na wapiga picha wakubwa walio bobea kutoka kila sehemu ya dunia, jumla ya kazi zilizo shindanishwa katika mashindano haya zilikua (6000), washiriki wa shindano hilo wametoka katika nchi (77), hafla ya kutoa zawadi imefanyika katika mji mkuu wa Urusi Mosco, miongoni mwa washindi na wakabidhiwaji wa zawadi ni bwana Taisiri Mahdi aliye kaiwakilisha Iraq katika mashindano hayo ya kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: