Vinaenda wapi vipande vya marumaru vinavyo tolewa katika sakafu na kuta za haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)?

Maoni katika picha
Mazuwaru na kila anaye fuatilia ujenzi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, anajiuliza vinaenda wapi vipande vya marumaru vinavyo tolewa katika sakafu na kuta za haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kwa ajili ya kujibu swali hilo tumeifuata kamati inayo husika na kutunza vipande hivyo ambavyo huchukuliwa kuwa ni vyenye thamani kubwa, vimehifadhiwa miaka na miaka katika kitendo cha zawadi na nadhiri kwenye idara ya marumaru, tumeongea na mkuu wa idara hiyo, Ustadh Maitham Razaaq Ni’imah ambaye amesema kua: “Zaidi ya muongo mmoja sasa tangu kazi ya ujenzi na ukarabati ishike kasi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, tulipata fikra ya kunufaika na vipande vya marumaru vinavyo tolewa wakati wa ujenzi na kuvitumia kwa kufanyia tabaruku, tunavitengeneza katika muonekano mzuri na huwa tunawapa mazuwaru wanaokuja kufanya ziara za Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kua: “Uandaaji wa marumaru hizo hupitia hatua kadhaa, kuna hatua ya kuzisafisha, hatua ya kuziweka nakshi na kuzichora chini ya mafundi walio bobea katika kazi hiyo, halafu hufuatia hatua ya kuzikata kisha kuzipaka rangi na kuziandika, thamani yake hutokana na mahala zilipo tolewa pamoja na wakati, kuna ambazo zinatengenezwa pete na mikufu, na zingine zinakatwa vipande vidogo vidogo na vya saizi ya kati”.

Akamaliza kwa kusema kua: “Hakika vitu vivyo hupewa zaairu kwa lengo la kutabaruku, kuna kiwango kidogo cha pesa ambazo zaairu hutakiwa kulipa na pesa huzo hupelekwa kufanya kazi za ndani ya Ataba tukufu, na baadhi yake hutolewa bure kwa mazuwaru na wageni wa Ataba”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: