Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na mwakilishi wa Iraq katika kituo cha tafiti za kihistoria na kiutamaduni kilicho chini ya umoja wa kiislamu chenye makao makuu katika mji wa (Ircica) Uturuki wamejadiliana namna ya kuongeza ushirikiano baina yao.
Hayo yamesemwa katika ziara iliyo fanywa na Dokta Salama Khafaji ambaye ni mwakilishi wa Iraq, katika maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya, na akakagua vituo vilivyo chini yake pamoja na kusikiliza maelezo kutoka kwa wasimamizi wa vituo hivyo, kabla ya matembezi hayo alikutana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Muhammad Ashiqar, walijadiliana kuhumsu mambo muhimu yatakayo fanywa na kituo katika mwaka wa (2019m), maktaba na Daru Makhtutwaat zinatarajia kufanya harakati tofauti, ikiwa ni pamoja na kufanya semina za Qur’ani, historia ya kiislamu, turathi na ujenzi pamoja na fani zingine za kiislamu, ikiwa ni pamoja na kuendeleza hati za kuandika kwa mikono na maktaba ya kielektronik.
Mheshimiwa katibu mkuu alionyesha kufurahishwa na mkakati huo na akaonyesha kua Atabatu Abbasiyya tukufu ipo tayali kutekeleza ratiba hiyo kwa faida ya pande zote mbili. Baada ya Dokta Khafaji na ujumbe alio fuatana nao pamoja na Dokta Hamidi ambaye ni mwakilishi wa wizara ya mambo ya nje ya Iraq kutembelea sehemu mbalimbali pamoja na makumbusho ya Alkafeel, walionyesha kufurahishwa na kazi nzuri inayo fanywa na vitengo vya makumbusho ambayo inakidhi vigezo vya kimataifa, na juhudi ya kulinda na kuhifadhi turathi za kiislamu kwa ujumla na turathi za Iraq, akabainisha kua: “Tumeona kazi nzuri na tunatamani kuitangaza kwa walimwengu, hakika watumishi wanauwezo wa hali ya juu wanakidhi vigezo vya kimataifa, kwa kweli jambo hili ni fahari na utukufu kwetu kama taifa, na sisi kama taasisi na ukizingatia Iraq ni mjumbe wa mkutano wa idara ya Ariska”.
Kumbuka kua kituo cha utafiti wa historia na utamaduni wa kiislamu (Ariska) kilichopo Istambul, kinatokana na kongamano la kiislamu na taasisi za kimataifa, kinaundwa na wajumbe kutoka nchi (57), kilianzishwa tangu mwaka (1980) kinajihusisha na kufanya utafiti katika mambo ya kimazingira, utamaduni na historia ya nchi za kiislamu, pamoja na historia za fani mbalimbali na athari za ujenzi na hati za kuanzika kwa mkono sambamba na kulinda turathi na utamaduni na kuziendeleza.