Mkuu wa shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa na viwanda Muhandisi Maitham Bahadeli amesisitiza kua, lengo la kushiriki maonyesho ya kimataifa ya Bagdad ya awamu hii sambamba na mashirika mengine ya kitaifa na kimataifa, ni kufikisha ujumbe wa wazi kua Iraq inauwezo na utaalamu mkubwa kiasi inaweza kuchuana na nchi kubwa katika uzalishaji, iwapo wataalamu wake wakipewa nafasi na wakiwezeshwa wanaweza kuinua taifa kiviwanda”.
Ameyasema hayo alipo kutana na ujumbe wa mtandao wa kimataifa Alkafeel, akaongeza kua: “Hii ni mara ya nne tunashiriki katika maonyesha haya ya Bagdad yanayo lenga kuonyesha mambo ya uchumi yasiyo julikana kwa raia wengi, Atabatu Abbasiyya tukufu inavitu vingi, inatoa huduma mbalimbali za kijamii, kiutamaduni, kibinaadamu hali kadhalika inasekta za kiuchumi, zinazo lenga kuinua uchumi kupitia mambo tofauti, inashiriki katika maonyesho haya kupitia sekta za biashara, viwanda na huduma, yato yanalenga sekta ya uchumi”.
Akabainisha kua: “Katika tawi letu tunaonyesha bidhaa zinazo tengenezwa na shirika la Aljuud, baadhi ya bidhaa hizo zina hati miliki ya shirika, bidhaa zetu sio za aina moja, tuna bidhaa zinazo husu sekta ya kilimo na sekta ya ufugaji, tunatengeneza mbolea za aina tofauti, na chembechembe hai za kibaiolojia zisizo kua na kemikali na salama sambamba na vifaa mbalimbali ambavyo vinatumika katika sekta ya tiba na bidhaa zingine nyingi nafasi haitoshi kutaja kila kitu”.
Tawi hili linapokea watu wengi wanao tembelea maonyesho haya na kufika katika meza yetu kuangalia bidhaa, pia bidhaa zetu ni jibu kwa mashirika ya serikali na mashirika ya kitaifa kua tunao uwezo wa kutengeneza bidhaa bora na zikatoa ushindani mkubwa duniani, pia bidhaa zinazo endana na mazingira ya Iraq, bidhaa zetu zimeonyesha mafanikio makubwa.
Kumbuka kua ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyesho haya ni mwendelezo wa ushiriki wake katika siku za nyumba ambao ulikua na mafanikio makubwa, mara hii imeshiriki kupitia matawi nane, ya viwanda, kilimo na chakula, ambayo ni: (Kundi la vitalu vya Alkafeel, Shirika la bidhaa za wanyama Nurul-Kafeel, Shirika la ujenzi, viwanda na biashara Lliwaaul-Aalamiyya, Darul-Kafeel ya uchapaji na usambazaji, Shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud, Shirika la usalama na mawasiliano Alkafeel, Shirika kuu la kiuchumi lililo chini ya kitengo cha kilimo na mifugo na Hospitali ya rufaa Alkafeel).