Apongeza utendaji wao: Sayyid Swafi akutana na jopo la wanahabari wa Atabatu Abbasiyya tukufu walio pewa jukumu la kutangaza ziara ya Arubaini na apongeza utendaji wao…

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amepongeza kazi nzuri iliyo fanywa na wanahabari waliokua wanatangaza ziara ya Arubainiyya chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, akawasisitiza kuongeza juhudi na kuhakikisha wanatumia vyombo vyote vya habari.

Aliyasema hayo kwenye kikao walicho fanya ndani ya ukumbi wa wageni wa Ataba, na kuhudhuriwa na katibu mkuu Muhandisi Muhammad Ashiqar pamoja na rais wa kitengo cha habari na utamaduni Sayyid Liith Mussawi na wasaidizi wake, baada ya ukaribisho na kusikiliza maelezo kutoka kwa wanahabari kuhusu mbinu walizo tumia katika kutangaza matukio ya ziara ya Arubaini ya mwaka huu, kiongozi mkuu wa kisheria akazungumza mambo kadhaa, miongoni mwa aliyosema ni:

 • 1- Katika mapinduzi ya bwana wa mashahidi (a.s) sekta ya habari ilikua na umuhimu mkubwa kwenye vita ya Twafu, katika siku ya kumi (Ashura) alisimamia sekta hiyo yeye mwenyewe kupitia khutumba mbalimbali alizo lihutubia jeshi la Yazidi.
 • 2- Watu wengi walifikiwa na habari potofu zikawafanya wasiende kumnusuru Imamu Hussein (a.s) na kuungana naye.
 • 3- Imamu Sajjaad na bibi Zainabu (a.s) walifanya kazi kubwa sana ya kueneza habari baada ya vita ya Twafu, tukio hili limetufikia hadi sisi kwa utukufu wao.
 • 4- Kuna haja ya kusoma kwa kina mambo yanayo husu ziara ya Arubainiyya na kuyatangaza katika vyombo vya habari.
 • 5- Inatakiwa kuwahimiza waumini kufanya ziara hii na kuelezea malengo yake matukufu kwa nguvu zote.
 • 6- Kwa kiasi tunavyo fanya katika vyombo vyetu vya habari, kama kuonyesha filamu, matukio ya moja kwa moja, kuonyesha hisia za mazuwaru, ndio tutakavyo weza kuvutia vyombo vingine vya habari vya kimatafa na kuja kutangaza matembezi ya Arubaini, jambo hili linategemea nguvu tutakayo tumia katika vyombo vyetu vya habari.
 • 7- Kuna vyombo vya habari huzusha matukio na kuyatangaza kwa nguvu sana ili watu wasifuatilie kinacho engelea katika ziara ya Arubaini, na ulimwengu usijue kitu, njama kama hiyo ilifanywa na Bani Umayya, wakati vita inaendelea katika ardhi ya Twafu watu wengi wa Kufa walikua hawajui kama kuna vita.
 • 8- Mnatakiwa kufanya maendeleo mapya ya kuitangaza ziara ya Arubaini kila mwaka kupitia uzowefu wenu.
 • 9- Mnajukumu la kuitangaza ziara ya Arubaini kwa walimwengu na kwa njia inayo stahiki.
 • 10- Kunaumuhimu wa kuwa na uhusiano wenye misingi madhubuti katika urushaji matukio ya ziara kwa walimwengu.
 • 11- Kutoweka vizuwizi vingi katika kuwapa nafasi wanahabari wa luninga zinazo taka kurusha matukio ya moja kwa moja (mubashara) katika ziara ya Arubainiyya,
 • 12- Ushirikiano wenu ni kitu kizuri sana, ndio sababu ya kufanikiwa kwa matangazo ya ziara ya Arubainiyya.

Mwisho wa kikao hicho Mheshimiwa Sayyid Swafi aliwataka watumishi wa sekta hii waanze maandalizi na kuweka mikakati ya namna watakavyo tangaza ziara ya Arubaini ijayo, akawaombea kazi zao zikubaliwe mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu na Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: