(Tumeanzia ulipoishia uchapishaji) kauli mbiu ya Darul Kafeel ya uchapishaji na usambazaji kwenye maonyesho ya Bagdad ya kimataifa…

Maoni katika picha
Tumeanzia ulipoishia uchapishaji, na tunafanya juhudi kuimarisha uchumi wa Iraq, huu ndio ujumbe wa Darul Kafeel ya uchapishaji na usambazaji, ambayo ni miongoni mwa matawi ya Atabatu Abbasiyya tukufu yanayo shiriki katika maonyesho ya kimataifa awamu ya (45).

Kiongozi wa tawi la Darul Kafeel katika maonyesho hayo, Ustadh Duredi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika ushiriki wetu unaendelea katika maonyesho ya Bagdad ya kimataifa na kwenye maonyesho mengine kwa ajili ya kutambulisha kazi zinazo fanywa na Darul Kafeel na matokeo yake katika eneo la mashariki ya kati, sambamba na kazi ya uchapishaji inayo fanywa na Darul Kafeel.

Akaongeza kua: “Tunaonyesha kazi muhimu za uchapishaji zilizo fanywa na Darul Kafeel, ukiwemo uchapishaji wa ubora wa juu kabisa, uchapishaji wa namba na uwekaji kava kitaalamu, pia tunaonyesha uwekaji wa dhahabu wa kawaida unao tumika, na namna ya kukata vitabu vinavyo chapishwa kwa kufuata mchoro wake”.

Akabainisha kua: “Pia limeandaliwa daftari kwa ajili ya kuonyesha hati mbalimbali na ukubwa wake, jambo hili linafanyika kwa mara ya kwanza mashariki ya kati, kwa maana hiyo ni muhimu sana kushiri Darul Kafeel katika maonyesho haya ambayo kuna mashirika mengi ya kitaifa na kimataifa yanayo shiriki”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki katika maonyesho haya kupitia matawi nane ambayo ni:

  • 1- Kundi la vitalu vya Alkafeel.
  • 2- Shirika la biashara Nurul-Kafeel.
  • 3- Shirika la ujenzi, viwanda na biashara Lliwaaul-Aalamiyya.
  • 4- Darul-Kafeel ya uchapaji na usambazaji.
  • 5- Shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud.
  • 6- Shirika la usalama na mawasiliano Alkafeel.
  • 7- Shirika kuu la kiuchumi lililo chini ya kitengo cha kilimo na mifugo.
  • 8- Hospitali ya rufaa Alkafeel.

Kitengo cha usimamizi wa kihandisi kumefanya kazi ya kutengeneza sehemu ya maonyosho ya kila tawi kutokana na aina ya vitu vinavyo onyeshwa na tawi husika, chini ya usimamizi wa kituo cha Alkafeel cha uchapaji wa namba wote wakiwa chini ya kitengo cha habari na utamaduni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: