Kikosi cha wapiganaji cha Abbasi kimetaja mkakati wa kuimarisha usalama na kutoa huduma katika ziara ya Maimamu wawili Askariyyaini (a.s)…

Maoni katika picha
Viongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kimetaja mkakati wa kuimarisha ulinzi na kutoa huduma kwenye ziara ya Imamu Hassan Askariy (a.s) katika siku ya kumbukumbu ya kifo chake itakayo fanyika Ijumaa ijayo (8 Rabiul Awwal 1440h).

Jambo hili ni katika mkakati wa ulinzi na utowaji wa huduma katika ziara za kidini, jambo linalo pewa umuhimu mkubwa na kikosi hiki baada ya kumaliza vita na magaidi wa Daesh mwaka jana.

Kimesema kua kitatumia askari wa akiba waliopo mikoani pamoja na kitengo cha rada, ili kuimarisha usalama katika ziara ya Atabatu Askariyya tukufu wakati wa kumbukumbu ya kifo cha Imamu wa kumi na moja Hassan bun Ali Askariy (a.s).

Kuhusu utowaji wa huduma, idara ya misaada ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imesema kua itakua na zaidi ya maukibu kumi za kuhudumia mazuwaru, pamoja na aina zingine za huduma zitakazo tolewa kwa mazuwaru watukufu.

Kumbuka kua kikosi cha Abbasi (a.s) kilikusanya maoni kutoka kwa mazuwaru kwa njia ya kielektronik katika ziara iliyo pita ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), miongoni mwa maoni hayo kuna yalio omba kuundwa kamati tatu kwa ajili ya ziara zinazo hudhuriwa na mamolioni ya watu zitakazo jitolea kulinda Ataba na maeneo matakatifu, kama sehemu ya kujiandaa kupeleka ombi hilo katika bunge la Iraq na serikali kuu siku zijazo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: