Kwa ajili ya kuweka mazingira bora ya utowaji wa huduma: Hospitali ya Alkafeel imeunda kitengo cha dharura kwa ajili ya kupokea watu walio katika hali mbaya…

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imefungua kitengo cha dharura kwa ajili ya kupokea watu walio katika hali mbaya, kina wabobezi wa magonjwa ya tumbo, moyo, kifua, majeraha, sumu na kuvunjika viungo, kwa ajili ya kutoa matibabu ya lazima na haraka kwa wenye marandi tuliyo taja.

Hatua hii imechukuliwa kwa ajili ya kuboresha huduma na kuhakikisha zinaendana na maendeleo ya kisasa katika sekta ya matibabu duniani, sambamba na kuboresha vitengo vya hospitali na kutoa huduma bora kwa ujumla, na kuhakikisha hakuna msongamano kama uliopo katika hospitali za serikali wakati wa kupokea wagonjwa wenye hali mbaya.

Uongozi wa hospitali umesema kua; wagonjwa wanapokelewa na jopo la madaktari wenye uwezo mkubwa wa kutibu aina mbalimbali za maradhi yanayo hitaji matimabu ya haraka.

Kwa maelezo zaidi unaweza kutembelea ofisi ya maelezo au kupika simu za kitengo cha mawasiliano cha hospitali ambazo hua wazi kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa mbili jioni, katika namba zifuatazo: (07602344444 / 07602329999 / 07730622230).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: