Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu: Ataba tukufu za Iraq zimejikita katika kuwahudumia mazuwaru na jamii kwa ujumla…

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Muhammad Ashigar amesema kua, Ataba huwahudumia mazuwaru watukufu kisha huelekea katika kuhudumia jamii kwenye sekta mbalimbali, ameyasema hayo alipotembelea matawi ya Ataba tukufu (Alawiyya, Kadhimiyya na Abbasiyya) yanayo shiriki katika maonyesho ya Bagdad ya kimataifa awamu ya (45) yanayo fanyika chini ya kauli mbiu isemayo: (Tumekusudia kujenga kama tulivyo komboa na kushinda).

Akaongeza kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi imekua ikishiriki katika maonyesho ya Bagdad ya kimataifa, hii ni mara ya nane inashiriki mfululizo”.

Akasisitiza kua: “Lengo la kushiriki kwetu ni kuonyesha ni bidhaa zetu hali kadhalika na bidhaa za Ataba zingine, kwani Ataba zumejikita katika kuhudumia mazuwaru watukufu pamoja na jamii kwa ujumla”.

Akaongeza kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki maonyesho haya kwa kuonyesha bidhaa zinazo tengenezwa na shirika la Aljuud, ambalo ni shirika la kiiraq linalo endeshwa na raia wa Iraq na linatengeneza bidhaa bora na salama pia ni rafiki wa mazingira, vilevile tunaonyesha bidhaa zinazo tengenezwa na shirika la uchumi Alkafeel, nalo ni shirika maarufu hapa nchini, linatengeneza bidhaa za viwandani, kilimo na wanyama, imeshiriki pia Darul Kafeel ya uchapishaji na usambazaji, pamoja na bidhaa za Nurul Kafeel na shirika la Lliwaaul Aalamiyya linalo tengeneza bidhaa za ujenzi zenye ubora wa hali ya juu, kutokana na ushahidi wa watumiaji wa bidhaa hizo, pamoja na shirika la usalama Alkafeel linalo jihusisha na mawasiliano, tunamshukuru Mwenyezi Mungu asilimia kubwa ya watu wanaotembelea maonyesho haya wamekua wakiyapongeza matawi ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akabainisha kua: “Ushiriki wa hospitali ya Alkafeel mwaka huu katika maonyesho haya ni kwa ajili ya kuonyesha uwezo wa hospitali hiyo katika kutibu magonjwa tofauti hapa Iraq chini ya madaktari wa kiiraq na wakigeni, inalenga kupunguza tabu kwa raia wa Iraq na kupunguza gharama za kufuata matibabu nje ya Iraq”.

Akafafanua kua: “Hospitali inatoa misaada mingi ya kibinaadamu ikiwa ni pamoja na kutibu bure au kwa punguzo watoto wa mashahidi, mafukara, majeruhi, watu wenye ulemavu na mayatiba, pia hospitali inamradi wa kwenda katika miji tofauti kutoa huduma za matibabu bure kwa mafakiri”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki katika maonyesho ya Bagdad ya kimataifa kupitia matayi nane ambayo ni:

  • - Kundi la vitalu vya Alkafeel.
  • - Shirika la biashara Nurul-Kafeel.
  • - Shirika la ujenzi, viwanda na biashara Lliwaaul-Aalamiyya.
  • - Darul-Kafeel ya uchapaji na usambazaji.
  • - Shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud.
  • - Shirika la usalama na mawasiliano Alkafeel.
  • - Shirika kuu la kiuchumi lililo chini ya kitengo cha kilimo na mifugo.
  • - Hospitali ya rufaa Alkafeel.

Kitengo cha usimamizi wa kihandisi kumefanya kazi ya kutengeneza sehemu ya maonyosho ya kila tawi kutokana na aina ya vitu vinavyo onyeshwa na tawi husika, chini ya usimamizi wa kituo cha Alkafeel cha uchapaji wa namba wote wakiwa chini ya kitengo cha habari na utamaduni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: