Atabayu Abbasiyya tukufu yawekwa mapambo meusi kwa ajili ya kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s)…

Maoni katika picha
Mazingira ya huzuni yametanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kuta na korido zake zimewekwa mapambo meusi kwa ajili ya kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s), bendera za maombolezo zimepandishwa na kuwekwa mabango yenye ujumbe wa kuomboleza ndani ya uwanja wa haram tukufu, kama alama ya huzuni waliyo nayo waumini na kumpa pole Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s).

Kama kawaida ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika kila tukio la kukumbuka kifo cha Ahlulbait (a.s), imeandaa ratiba maalumu ya maombolezo haya yenye vipengele vingi, kutakua na utowaji wa mihadhara ya Dini, ufanyaji wa majlis za kuomboleza pamoja na kufanya matembezi ya pamoja baina ya Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya kwa ajili ya kuomboleza msiba huu.

Kumbuka kua wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kila sehemu ya Dunia huomboleza msiba huu na kumpa pole Imamu wa zama Hujjat bun Hassan (a.f), kutokana na kifo cha baba yake Imamu Hassan Askariy (a.s), aliye uwawa na mtu muovu zaidi, alipewa sumu kali na Mu’tamad Abbasiy iliyo haribu mwili wa Imamu (a.s), akalala kitandani siku kadhaa akiwa na machungu makali kutokana na sumu hiyo, Imamu alifariki akiwa na umri wa miaka ishirini na nane, tarehe nane Rabiul Awwal mwaka (260h).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: