Baada ya kuona ubora wa kazi zake: Benki kuu ya Iraq yasaini mkataba na Darul Kafeel ya uchapaji na usambazaji kwa ajili ya kuchapiwa baadhi ya nyaraka zake…

Maoni katika picha
Katika maonyesho ya Bagdad ya kimataifa awamu ya (45) Darul Kafeel ya uchapaji na usambazaji ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imesaini rasmi mkataba na benki kuu ya Iraq kwa ajili ya kuichapia baadhi ya nyaraka zake muhimu katika utendaji wa benki.

Maonyesho hayo yalifunguliwa siku ya Jumamosi iliyo pita chini ya kauli mbiu isemayo: (Tumeazimia kujenga kama tulivyo komboa na kushinda) katika uwanja wa maonyesho ya kimataifa wa Bagdad. Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki kupitia matawi nane, miongoni mwa matawi hayo ni tawi la Darul Kafeel ya uchapaji na usambazaji, ambayo imetumia kauli mbiu isemayo: (Tumeanzia ulipoishia uchapishaji na tunafanya kazi ya kujenga kujitegemea na kukuza uchumi wa Iraq).

Maendeleo makubwa katika fani ya uchapaji yameshuhudiwa na kila aliye tembelea tawi la Darul Kafeel ya uchapaji na usambazaji, uwezo wa wafanya kazi, ubora wa vifaa vilivyopo, yote hayo yameboresha utendaji na kufikia kiwango cha kimataifa, jambo ambalo halikufikiwa na taasisi nyingi za uchapaji na usambazaji kwa muda mrefu.

Vifaa vya kisasa tulivyo navyo na utaalamu wa watumishi wetu vimezivutia baadhi ya taasisi za serikali kuingia mikataba rasmi na sisi kwa ajili ya kuwachapia baadhi ya nyaraka zao muhimu, miongoni mwa kazi tulizo pewa ni kuchapisha vitabu vya kufundishia vilivyopo kwenye mtaala wa shule za Iraq.

Tunapenda kuwafahamisha kua tawi la Darul Kafeel la uchapaji na usambazaji katika maonyesho haya, linaonyesha baadhi ya machapisho muhimu na huduma wanazo toa, kama uchapishaji kwa kutumia rangi za msingi, uchapishaji wa kiwango bora zaidi, pamoja na uchapishaji wa kufuata namba, uwekaji kava wa kisasa, pia tunaonyesha namna ya kutumia wino wa dhahabu katika kuandika, na tumeonyesha mfano wa kukata maumbo na machapisho kwa kufuata mchoro.

Kumbuka kua kuanzishwa kwa mradi wa Darul Kafeel ya uchapaji na usambazaji ni miongoni mwa mkakati wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kujitegemea katika sekta ya uchapishaji wa vitabu, majarida na magazeti, na kuhimiza utamaduni wa kusoma jambo ambalo humnufaisha muandishi na msambazaji pia, tumejitahidi kuongeza ubora na kupunguza gharama, tunatumia vifaa vya kisasa kabisa vinavyo kubalika kimataifa, kwa ajili ya kukidhi haja ya Ataba tukufu na taasisi zingine katika swala la uchapaji wa vitabu, majarida na magazeti yenye ubora wa hali ya juu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: