Mradi wa kufuta ujinga katika Atabatu Abbasiyya tukufu wakamilisha hatua ya kwanza na wajiandaa kupokea wanafunzi…

Maoni katika picha
Baada ya kupasishwa mradi wa kufuta ujinga unao tekelezwa na Atabatu Abbasiyya kwa kufundisha masomo ya msingi, sasa wapo mwishoni mwa maandalizi ya hatua nyingine ya masomo, nayo ni hatua ya kukamilisha masomo ya hatua ya awali ambayo ndio mlango wa kuelekea katika ngazi zingine za masomo, tayali wanafunzi (58) wamefanya mtihani wa kumaliza kwenye vituo vilivyo funguliwa na Ataba tukufu katika mkoa wa Karbala, wanasubiri majibu ambayo wanatarajia kufaulu kwa kiasi kikubwa.

Mkuu wa mradi huu Ustadh Muhammad Abdu Ridha Mussawiy ametuambia kuhusu mradi huu kua: “Mradi wa kufuta ujinga kwa kusomesha (kusoma na kuandika) ni miongoni mwa miradi ya kielimu inayo endeshwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, ambao unalenga kuwasadia watu wasio jua kusoma (ambao hawawezi kusoma na kuandika), na kuwafanya wapate elimu itakayo wasaidia waishi vizuri katika jamii, na kuwatoa katika giza la ujinga (kutojua kusoma na kuandika), tunamshukuru Mwenyezi Mungu mwitikio ni mzuri sana, na wanafunzi wataweza kumaliza hatua mbili za msingi katika masomo haya (ya msingi), baada ya kufanya mitihani ya mwisho waliyo pewa na idara ya tarbiyya ya mkoa wa Karbala / kitengo cha kufuta ujinga, ambapo zowezi hilo lilifanyika baada ya kuwasiliana na wasimamizi wa mradi huu, ambapo idadi ya wanafunzi walio fanya mitihani hiyo ni (58)”.

Akaongeza kua: “Baada ya kufaulu mitahani hiyo watapewa vyeti vinavyo tambuliwa na wizara ya Tarbiyya (cheti cha kujua kuandika na kusoma) ambacho ni cheti cha darasa la nne la shule ya msingi, lakini masomo yetu hayaishii katika awamu hizo mbili peke yake, bali tumeweka kiwango cha juu kwa wanaotaka kuendelea na masomo, tunaweza kuwaingiza katika hatua ya darasa la tano, ambapo wataweza kuendelea hadi darasa la sita na kupata cheti cha kuhitimu elimu ya msingi”.

Akabainisha kua: “Tulianza nao katika hatua ya mwanzo kabisa (sifuri) na sasa hivi wanajua kusoma na kuandika, tuna maombi mengi ya watu wanaotaka kujiunga na masomo haya, tunasubiri kukamilika kwa maandalizi ya kiutawala ili tuanze kuwafundisha, katika vituo tulivyo fungua kwenye wilaya na vitongoji mbalimbali pamoja na makao makuu ya mradi ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Kumbuka kua mradi huu huanza kutekelezwa baada ya kupewa ruhusa na wizara ya Tarbiyya ya Iraq, kwa kushirikiana na ofisi ya Tarbiyya ya mkoa wa Karbala, chini ya walimu wazowefu walio teuliwa kwa ajili ya ufundishaji katika mradi huu, sambamba na kuandaa sehemu maalumu za kufundishia, tumeteua baadhi ya husseiniyya na majengo yaliyopo ndani ya mkoa wa Karbala kama sehemu za kuendeshea masomo haya, cheti cha kufuta ujinga wanapewa baada ya kumaliza darasa la nne la shule ya msingi, ambapo wanafanya mtihani kutoka wizarani na kupewa vyeti na wizara vinavyo tambuliwa na serikali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: