Miongoni mwa yaliyo thibitishwa katika uliwazaji wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ndugu yake Hussein (a.s), katika ziara yake maarufu iliyo pokewa na Imamu Swadiq (a.s) kuna kipengele kinasema: (Nashuhudia ulinasihi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na ndugu yako, ndugu mora mliwazaji), hii ni sifa tukufu zaidi kwake, aliyo itaja Imamu Swadiq (a.s) kwa ammi yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Hakua Imamu Swadiq (a.s) peke yake aliye mpa ammi yake Abulfadhil Abbasi (a.s) sifa hiyo, pia Imamu Haadi (a.s) alifanya kama alivyo fanya babu yake Imamu Swadiq (a.s), akamwita ammi yake Abbasi (a.s) kwa sifa hiyo, katika ziara iliyo pokelewa mwaka wa miambili hamsini na mbili hijiriyya, kuna kipengele kinasema: (Amani iwe juu ya Abulfadhil Abbasi, mliwazaji wa ndugu yake, aliyetumia kesho yake katika jana yake, aliye mtosheleza, aliye kwenda kuleta maji, aliye katwa mikono yake).
Ni wazi kua Abulfadhil Abbasi (a.s) kupewa sifa ya uliwazaji na Maimamu wawili maasumina, sifa hiyo imepasishwa na Mwenyezi Mungu mtukufu, pia ni ushahidi wa wazi wa umakini wa hali ya juu aliokua nao Abulfadhil Abbasi (a.s) katika Dini, na namna alivyo kua akiitambua haki ya Imamu wake, na ikhlasi aliyo kua nayo katika kumliwaza.