Kwa nini watu wasimiminike na machozi yasibubujike, wakati anayepewa pole ni Imamu wa Zama Imamu Hujjat bun Hassan (a.f), hawa hapa answari wake wanaelekea Samara tukufu kumpa pole kutokana na kumbukumbu ya kifo cha baba yake Askariy (a.s).
Mji mtukufu wa Samara umeshuhudia malaki ya waumini kutoka mikoa tofauti ya Iraq na nje ya Iraq, wakielekea katika malalo ya Maimamu wawili Ali Haadi na Hassan Askariy (a.s) katika kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s), aliyefariki (8 Rabiul Awwal 1440h), watu walianza kumiminika tangu siku nne zilizo pita na kilele cha ziara ni mchana wa leo siku ya Ijumaa inayo sadifu tarehe ya kifo chake.
Atabatu Askariyya tukufu imetumia uwezo wake wote kuhakikisha ziara hii inafanyika kwa amani na utulivu kwa kushirikiana na Ataba zingine za Iraq, chini ya ratiba maalumu na kwa kushirikiana na wanajeshi wa serikali pamoja na wale wa Hashdi Sha’abi wanaolinda usalama katika eneo hilo.
Mawakibu za kutoa huduma –kama kawaida yao- zimeenea ndani ya mji wa Samara na katika njia zinazo elekea kwenye mji huo, kwa ajili ya kutoa huduma za chakila, vinywaji, malazi na zinginezo kwa mazuwaru watukufu.
Ziara hii imefanyika kwa namna ya pekee kutokana na mafanikio ya wanajeshi wetu na Hashdi Sha’abi dhidi ya magaidi wa Daesh, na kukombolewa kwa ardhi yote iliyokua imetekwa na magaidi hao, hali hiyo imeakisi katika ziara hii, kwa kuongezeka idadi ya mazuwaru wanaokuja katika mji huu mtakatifu, ambao maadui wa Ahlulbait (a.s) walitaka kuwazuwia wafuasi hao wasije katika mji huu, Mwenyezi Mungu alikataa hilo, Nuru yake itaangaza daima hata kama washirikina wakichukia.