Vipengele muhimu vilivyo zungumzwa na Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa…

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s) leo (8 Rabiul Awwal 1440h) sawa na (16 Novemba 2018m) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, amezungumzia nukta nyingi, miongoni mwa nukta hizo ni:

  • - Batili wakati mwingine huwa ni batili kisheria na wakati mwingine sio kisheria bali kijamii.
  • - Vyovyote mwanaadamu atakavyo kua sawa awe na nguvu za kimwili au kimadaraka hatakiwi kufanya batili.
  • - Batili haiwezi kukufikisha mahala salama.
  • - Mwenye jukumu la kutoa huduma au kiongozi wa kabila hatakiwi kupanda mgongo wa batili.
  • - Ewe unayepanda mgongo wa batili ukiwa unajitambua yakupasa utafakari.
  • - Mwanaadamu anatakiwa kutumia hekima na kutofanya maamuzi ya haraka ili apande mgongo wa haki na sio batili.
  • - Haitoshi mtu kusema mimi ninahekima bali inatakiwa ionekane katika vitendo vyake.
  • - Mwanaadamu anatakiwa awe na msimamo na atumie akili.
  • - Nyumba ya majuto sio nyepesi na sio kila juto unaweza kulimudu.
  • - Kuna majuto yasiyo vumilika na umri haudumu hakuna anayejua lini atakufa.
  • - Umri hautoi nafasi ya kurekebisha yanayo baki, na kuna majuto husababisha maangamizi kwa mjutaji kwa sababu alipanda mgongo wa batili.
  • - Mwanaadamu anatakiwa kutumia akili, hekima na busara katika vitendo vyake, hasira zisimpelekee kufanya maovu.
  • - Mtu anaposikia jambo anatakiwa atafakari na kufanya subira.
  • - Kuhukumu mambo kwa pupa mwisho wake huwa ni majuto.
  • - Atakaye panda mgongo wa batili asimlaumu yeyote zaidi ya nafsi yake pale atakapo telemkia katika nyumba ya majuto.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: