Kuadhimisha kumbukumbu ya mazazi matakatifu: Atabatu Abbasiyya tukuf imetangaza wiki ya maadhimisho ya kuzaliwa kwa Mtume (s.a.w.w)…

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia Daru Rasuul A’dham (s.a.w.w) chini ya kituo cha utafiti na masomo Al-Ameed, imetangaza wiki ya maadhimisho itakayo kua na vipengele mbalimbali, kwa ajli ya kusherehekea kuzaliwa kwa muokozi wa wanaadamu, aliye kuja kuwatoa katika giza na kuwatia katika nuru Nabii mtukufu Muhammad (s.a.w.w).

Dokta Aadil Nadhiri Biri ambaye ni Rais wa Daru Rasuul A’dham (s.a.w.w) ameleza kuhusu maadhimisho hayo kua: “Wiki ya kiutamaduni ni moja ya harakati zitakazo fanywa na Daru, maadhimisho haya yanafanyika mahsusi kwa ajili ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume mtukufu (s.a.w.w), ratiba yake inahusisha Atabatu Abbasiyya na vyuo vikuu vitatu, itazinduliwa katika chuo kikuu cha Misaan siku ya Alkhamisi (22 Novemba) na yataendelea kufanyika ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Ijumaa, na katika chuo kikuu cha Bagdadi siku ya juma pili, na kumalizia katika chuo kikuu cha Karbala siku ya Jumatatu ya tarehe (26 Novemba 2018m).

Akaongeza kua: “Katika mnasaba huu Daru Rasuul A’dham (s.a.w.w) itafanya vikao vya kielimu vya kuelezea sira tukufu ya Mtume (s.a.w.w) sambamba na sifa zake na tabia zake takatifu, kwa ajili ya kuweka mazingira ya kielimu pamoja na kuutambulisha zaidi utukufu wa Mtume (s.a.w.w)”.

Akabainisha kua: “Kutokana na mnasaba huu tunatoa wito kwa kila mtu kuhudhuria vikao hivyo kwa ajili ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake watakasifu (a.s), na kuifanyia kazi kauli isemayo: (Huisheni mambo yetu Mwenyezi Mungu amrehemu atakaye huisha mambo yetu)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: