(Imamu Hussein (a.s) ni mnara wa umma na mrekebishaji wa maadili) ndio kauli mbiu ya awamu ya kumi na tano ya kongamano la Rabiu Shahada…

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada inaendelea kufanya vikao, chini ya utaratibu waliojiwekea tangu kuisha kwa kongamano lililopita, wamesha jadili mambo mengi yanayo husu kongamano lijalo, litakalo anza mwanzoni mwa mwezi wa Shabani ujao –Insha Allah-.

Kwa mujibu wa maelezo ya mjumbe wa kamati ya maandalizi na naibu rais wa kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya Sayyid Aqiil Abdulhussein Yasiriy, ambaye amesema kua: “Kamati ya maandalizi ya kongamano pamoja na baadhi ya wakuu wa vitengo wamefanya vikao kadhaa vya kujadili ratiba na kutoa mapendekezo kwa viongozi wakuu wa kisheria wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, ili waweze kuangalia mapendekezo hayo na kuyabariki au kutoa maoni yao, miongoni mwa mambo waliyo jadili ilikua ni kauli mbiu ya kongamano, zilipendekezwa kauli mbiu njingi na ikachaguliwa kauli mbiu isemayo: (Imamu Hussein (a.s) ni mnara wa umma na mrekebishaji wa maadili) kua kauli mbiu ya kongamano lijalo”.

Akaongeza kua: “kuchaguliwa kwa kauli mbiu hii kumetokana na uhusiano uliopo katika ujumbe huo na Imamu Hussein (a.s) pamoja na harakati yake tukufu, iliyo weka mizizi ya misingi ya uislamu na ubinaadamu na kuilinda isiharibiwe, kwa hiyo kongamano hili ni sehemu ya kuendeleza fikra za bwana wa mashahidi (a.s) katika kusahihisha uwelewa na maadili, kwa ajili ya kujenga jamii yenye umoja iliyo shikamana kifikra na kitabia na iliyo pambika na utamaduni wa Ahlulbait (a.s)”.

Kumbuka kua kongamano la kiutamaduni na kimataifa Rabiu Shahada husimamiwa na kugharamiwa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya tangu kuasisiwa kwake, ambalo hufanywa kwa ajili ya kuadhimisha kuzaliwa kwa mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) Imamu Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: