Katika ushiriki wake kwenye maonyesho ya Bagdad ya kimataifa: Shirika la Aljuud laonyesha bidhaa mpya na lasisitiza kua linaendelea kuziboresha na kukuza uzalishaji wa ndani…

Maoni katika picha
Shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud limeonyesha bidhaa mbalimbali linazo tengeneza, chini ya wataalamu ambao ni raia wa Iraq, katika maonyesho yanayo endelea Bagdad ya kimataifa, na kua shirika lenye mchango mkubwa katika utengenezaji wa bidhaa za ndani na kurudisha haiba ya viwanda vya Iraq.

Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Muhandisi Maitham Bahadeli ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Ataba tukufu zinaupekee maalumu katika kila jambo zinalo shiriki, chini ya uwelewa huo na kutokana na maelekezo ya Atabatu Abbasiyya inayo sapoti dhana hii, shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud limeonyesha bidhaa mpya ambazo ndio zimeingizwa sokoni kwa mara ya kwanza, bidhaa hizo ni:

  • - Jiki ya kuoshea sakafu banamatumizi yenye ujazo wa lita (3.250) na inaharufu tofauti za aina sita.
  • - Sabuni ya maji ya kuonshea sakafu yenye harufu za aina sita tofauti na ujazo mbalimbali inayo kidhi mahitaji ya familia za wairaq.
  • - Dawa ya kusafisha mdomo, inatoa mabaki ya vyakula na kuuacha mdomo ukiwa safi.
  • - Pamoja na bidhaa za viumbe hai pia kuna bidhaa mbili ambazo hutumika katika mazingira ya wanyama, na kufanya mazingira kua salama”.

Kumbuka kua tawi la shirika hili limepata mwitikio mkubwa kutoka kwa watu wanaokuja kutembelea maonyesho haya, na limekua jibu kwa mashirika ya serikali na mashirika binafsi kutokana na umuhimu wa bidhaa zake, na limeonyesha mafanikio makubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: