Maahadi ya Imamu Hussein (a.s) ya wahadhiri wa kike yaanza kusajili wanafunzi wapya…

Maoni katika picha
Maahadi ya Imamu Hussein (a.s) ya wahadhiri wa kike ambayo ipo chini ya idara ya wahadhiri wa kike ya Atabatu Abbasiyya tukufu yenye makao makuu ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), imetangaza kuanza usajili katika msimu mpya kwa wanaopenda kujiunga na jahazi la wahudumu wa mimbari ya bwana wa mashahidi (a.s), chini ya selebasi zinazo fatwa na shule zingine za aina hii.

Idara imebainisha kua usajili unaendelea katika ofisi ya Maahadi iliyopo karibu na mlango wa Imamu Mussa Alkadhim (a.s) ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika madrasa ya Darul Ilmi, kwa maelezo zaidi piga simu namba: (07810645244 au 07602334055), waombaji wa kujiunga na masomo hayo watapewa mtihani maalum wa majaribio ulio andaliwa na Maahadi, kisha wataingia katika masomo ya hatua ya awali ili kuwaandaa waweze kuendelea na hatua tatu za masomo zinazo fuata, kuna masomo ya Aqida, uhadhiri, nahaul-waadhiha, ibadaati, tafsiri ya Qur’ani, usomaji wa Qur’ani, siratu Nabawiyya pamoja na mazowezi ya utowaji wa mihadhara, tambua kua muda wa masomo ni miaka mitatu na wahitimu watapewa vyeti na Maahadi.

Idara imesema kua; mwaka huu inajiandaa kuongeza masomo mapya yatakayo saidia kukuza uwezo zaidi wa wahadhiri wetu na kuwafanya waendane na maendeleo ya jamii tunazo ishi, limeongezwa somo la (buhuthi fi siirah).

Kumbuka kua lengo la kuanzishwa kwa maahadi hii ni kuimarisha tablighi upande wa wanawake kutokana na umuhimu mkubwa walio nao hasa katika vipindi vya huzuni, na kuwatoa upenuni hadi katika uwanja mpana wa kuelezea tukio la milele la Imamu Hussein (a.s) kwa njia nzuri inayo eleweka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: