Mada zitakazo shidaniwa ni:
- 1- Islahi ya kiongozi na serikali kutokana na tishio, barua ya Imamu Hussein (a.s) kwa watu wa Kufa.
- 2- Islahi katika khutuba ya Imamu Hussein (a.s) baina ya nadhariyya na uhalisia.
- 3- Athari za mimbari ya Husseiniyya katika kujenga misingi ya tabia na kurekebisha jamii pamoja na kutangaza lengo.
- 4- Athari za urithi na malezi katika kujenga nguvu.. Abbasi (a.s) kama mfano.
- 5- Uelewa wa mafundisho ya Dini katika kupambana na fikra potofu katika upeo wa matukio ya Ashura.
- 6- Uelewa wa Islahi.. hukumu na kanuni zake.
- 7- Misingi mikuu kifikra katika dua ya Arafa.
- 8- Athari za maadhimisho ya Husseiniyya katika kujenga misingi ya tabia na imani.
- 9- Uhusiano wa kifamilia na kibinaadamu katika madrasa ya Ashura.
- 10- Athari ya kutakasa nafsi katika kusambaza misingi ya Islahi.. Imamu Sajjaad (a.s) kama mfano.
- 11- Makusudio na kukubalika katika maneno ya Imamu Hussein (a.s): (Mimi sijui wafuasi bora na waaminifu zaidi ya wafuasi wangu).
Kamati ya maandalizi imeweka masharti na kanuni zinazo takiwa kufatwa na watafiti watakao shiriki katika shindano la kongamano hilo, ambayo ni haya yafuatayo:
- 1- Utafiti usiwe umeshawahi kutolewa au kusambazwa na watu wengine kabla yako.
- 2- Uandikwe kwa kufuata vigezo vya kielimu.
- 3- Usiwe chini ya kurasa (20) na sio zaidi ya (30) uandikwe kwa hati ya (Arabic simplified) ukubwa wa herufi uwe saidi (14) na uhifadhiwe kwenye (CD).
- 4- Usiwe na zaidi ya maneno (300), utafiti huo uambatane na muhtasari wake.
- 5- Hautakubaliwa utafiti wowote tofauti na mada tulizo tajwa au ambao hauta ambatanishwa na wasifu wa muandishi.
- 6- Tafiti pamoja na muhtasari na wasifu (cv) ya muandishi bapona na picha mbili ndogo na namba ya simu na anuani ya barua pepe zitumwe katika anuani ya kongamano la Rabiu Shahada ifuatayo: rabee@alkafeel.net.
- 7- Mwisho wa kupokea tafiti hizo ni mwanzoni mwa mwezi wa Rajabu (1440h) sawa na (9 Machi 2019m).
- 8- Kwa maelezo zaidi piga simu zifuatazo: (07728243600) au (07602428226).
Kamati imeandaa zawadi kwa washindi watatu wa mwanzo kama ifuatavyo:
Mshindi wa kwanza (1,500,000) milioni moja na laki tano dinari za Iraq.
Mshindi wa pili (1,000,000) milioni moja dinari za Iraq.
Mshindi wa tatu (750,000) laki saba na elfu hamsini dinari za Iraq.