Mwezi kumi Rabiul Awwal Mtume (s.a.w.w) alimuoa bi Khadija (a.s)…

Maoni katika picha
Mtume Mtukufu (s.a.w.w) kumuoa bi Khadija bint Kuwailid (a.s), kumbukumbu hiyo inasadifu siku ya leo, na lilikua tukio muhimu sana katika historia ya uislamu, kwani alikua na nafasi kubwa sana katika uhai wa Mtume na uislamu kwa ujumla, kabla ya Utume na baada yake, pamoja na kwamba ndoa hiyo ni tukufu kwa kuwakutanisha watu watakatifu lakini pia ilikua na faida kubwa katika uislamu.

Bibi Khadija (a.s) alikua mwanamke bora katika wanawake wa kikuraish, alikua na mali nyingi, mzuri wa sura, katika zama za ujinga alikua anaitwa Mtakasifu (Twahira) pia alikua anaitwa (Bibi wa Makuraishi), watu walikua wanaona fahari kuwa karibu yake.

Viongozi wakubwa wa Makuraishi walitaka kumuowa kwa kumuahidi mali nyingi lakini aliwakataa, akamchagua Mtume (s.a.w.w) kutokana na utukufu wake na tabia nzuri aliyo kua nayo, shuhuda nyingi zinaonyesha yeye ndiye aliye anza kuomba aolewe na Mtume (s.a.w.w), bibi Khadija (a.s) alikua sio mfuasi wa Dini ya watu wa Maka ya ushirikina, alikua anaamini Dini ya Nabii Ibrahim (a.s).

Abuu Twalib bamoja na watu wa nyumbani kwake wakaenda hadi kwa mzazi wa Bi Khadija ambaye ni ammi yake Amru bun Asadi, kwa sababu baba yake alikua amesha uwawa katika vita ya Fijjaar au kabla ya vita hiyo, wakamposa, miaka kumi na tano kabla ya Utume kwa kauli mashuhuri.

Bibi Khadija alikua nguzo muhimu kwa Mtume (s.a.w.w) alimsaidia mtume katika mazingira magumu zaidi, alijitolea mali zake zote kwa ajili ya uislamu, ndoa hii tukufu iliasisi misingi ya ubinaadamu na tabia njema, ikiwa ni pamoja na kusema kweli, kutekeleza amana. Miongoni mwa matunda ya ndoa hiyo tukufu, watoto wote wa Mtume (s.a.w.w) wamezaliwa na bibi Khadija (a.s) ispokua Ibrahim, yeye alizaliwa na Mariya Qibtwiyya, bibi Khadija (a.s) alimzaa: Qassim na Twayyib, ambao walikufa wakiwa bado wadogo katika mji wa Maka, na akamzaa Zainabu, Ummu-Kulthum, Ruqayya na Fatuma Zaharaa (a.s).

Vitabu vya historia vimethibitisha kua ndiye mwanamke wa kwanza kumuamini Mtume (s.a.w.w), mtu wa kwanza kuamini Utume wake alikua ni mke wake bi Bidija binti Khuwailid, na katika riwaya ya Ibun Abbasi inasema: “Watu wa kwanza kumuamini Mtume (s.a.w.w) ni mtoto wa Ammi yake Ali bun Abu Twalib na mke wake Khadija binti Khuwailid” bi Khadija alikua na heshima kubwa sana miongoni mwa wake wa Mtume (s.a.w.w), alikua na nafasi maalumu kwake, aliendelea kumtaja kwa kheri na kusisitiza utukufu wake wakati wote wa uhai wake (s.a.w.w), alimsifia daima na hakuona anaye fanana naye kwa utukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: