Katika mashirika zaidi ya (300) kutoka nchi za kiarabu na kiajemi yanashiriki katika maonyesho ya kimataifa ya Bagdad, tawi la shirika la amani Alkafeel limepata mwitikio mkubwa kutoka kwa watu wa jinsia na rika zoto…

Maoni katika picha
Mwaka wa kumi mfululizo shirika la mawasiliano Alkafeel linashiriki katika maonyesho ya kimataifa ya Bagdad, kutokana na imani waliyo nayo viongozi wa shirika hilo katika maonyesho haya na fursa ya kuonsha huduma wanazo toa, katika maonyesho haya ya kimataifa ambayo kuna mashirika zaidi ya (300) kutoka Iraq, nchi za kiarabu na zisizokua za kiarabu.

Mgurugenzi mtendaji wa shirika Mhandisi Aarifu Bahhaash ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tunawapongeza wairaq kwa hii fursa kubwa ya kiuchumi inayo ashiria maendeleo baada ya kupata ushindi, na kuifanya Iraq iimarike kiuchumi baada ya kushinda vita, na kuifanya Iraq isimame mahala pake kwa utukufu wa muhanga waliojitolea raia wake”.

Kuhusu ushiriki, Bahhaash amefafanua kua: “Shirika hutilia umuhimu mkubwa wa kushiriki katika maonyosho ya kimataifa ya Bagdad, hii ni fursa nzuri kwa wazalishaji na watumiaji, ni sehemu ambayo utafahamu bidhaa tofauti zinazo tengenezwa na watu au viwanda tofauti, katika tawi letu tunaonyesha njia za kisasa zaidi za mawasiliano sambamba na huduma za kisasa zinazo tolewa na wahandisi wa kitengo cha utafiti wa maendeleo”.

Akaongeza kua: “Hakika tawi la shirika hili limepata mwitikio mkubwa sana kutoka kwa watu wanaokuja kutembelea maonyesho haya, na tumekua tukiwafafanulia huduma zinazo tolewa na shirika kwa sasa, na mkakati wa maendeleo wa baadae”.

Mkurugenzi mkuu alifafanua siku za nyuma kua: “Hakika shirika linafanya kila liwezalo kwa ajili ya kuboresha huduma za mawasiliano kwa ajili ya kuwahudumia wateja wetu wanao onyesha uaminifu kwetu, bila kusahau kazi zote tunafanya chini ya maekekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, na kumpa nafasi raia ya kuangalia viwango vya bei za mashirika likiwemo shirika letu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: