Maahadi ya Qur’ani tukufu ya Atabatu Abbasiyya yatangaza mashindano ya mapambo pora zaidi yatakayo wekwa katika msahafu na kuchapishwa…

Maoni katika picha
Kituo cha maarifa ya Qur’ani, kuifasiri na kuichapisha katika Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza kufanyika mashindano ya mapambo mazuri zaidi yatakayo wekwa na kuchapishwa katika msahafu mtukufu utakao chapishwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetoa wito kwa wataalamu wa hati na waandishi wa mapambo waje kushiriki katika mashindano hayo.

Kituo kimeweka masharti ya fuatayo kwa washiriki:

  • 1- Mapambo ya ukurasa wa kwanza ambao unasurat Fat-ha na mapambo ya ukurasa wa pili ambao umeandikwa aya za mwanzo wa surat Baqara, pamoja na umbo na mpangilio wa sural Fat-ha sambamba na sura inayo fuata, eneo la sura liwe kubwa ili herufi ziwe wazi kwa usomaji.
  • 2- Mapambo ya ndani ya msahafu, hasa sehemu ya jina la sura na juzuu juu ya ukurasa, na sehemu za hizbu pembezoni mwa kurasa.
  • 3- Mapambo ya majina ya sura na namba za aya.
  • 4- Mapambo yatokane na yale yaliyopo katika Maqaamu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na yaendane na yale yaliyomo katika malalo yake tukufu.
  • 5- Ukubwa wa mapambo uwe wa sentimita 50/70.
  • 6- Kituo hakilazimiki kurudisha kazi itakayo shiriki kwa muhusika, kazi itakayo shinda nafasi ya kwanza itamilikiwa na Ataba tukufu.
  • 7- Kazi za washiriki zikabidhiwe kwenye kituo cha maarifa ya Qur’ani, kuifasiri na kuichapisha katika Maahadi ya Qur’ani tukufu mkabala na mgahawa (Mudhifu) wa Abulfadhil Abbasi (a.s) Karbala tukufu, mwisho wa kupokelewa kazi hizo ni siku ya Alkhamisi ya tarehe (10/1/2019m).
  • 8- Mshiriki anatakiwa awe raia wa Iraq.
  • 9- Kazi zitachambuliwa na kushindanishwa chini ya kamati ya machaji walio bobea katika kituo, kwa kufuata masharti tuliyo weka.
  • 10- Mshindhi wa kwanza atapewa zawadi ya dinari za Iraq milioni tatu.

Kwa maelezo zaidi pipa simu namba: (009647602323733) au tuma barua pepe kwenye anuani ifuatayo: M.t.t.q313@gmail.com .
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: