Chuo kikuu cha Al-Ameed chafanya hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wapya na chawatakia mwaka mwema wenye kujaa elimu…

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed kupitia kitengo cha malezi na elimu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wapya walio jiunga katika vitivo vyake vya (Udaktari, udaktari wa meno na uuguzi) kwa mwaka wa maosomo (2018/2019), hafla hiyo imefanyika ndani ya ukumbi mkuu wa chuo na kuhudhuriwa na viongozi, walimu na wanafunzi, imekua kawaida ya chuo hiki kila mwaka, kufanya hafla kama hii kwa ajili ya kuwakaribisha wanafuzi wapya na kuwaelezea ratiba na taratibu za chuo, kwa ajili ya kuwapa nafasi ya kuzowea mazingira ya chuo na kua wanafunzi bora.

Rais wa chuo Dokta Jaasim Marzuki katika ujumbe wake amewatakia mwaka mwema wa masomo ulio jaa elimu na maarifa, akawasisitizia kua chuo kitafanya kila kiwezalo kupitia idara na watumishi wake kuhakikisha kinawawekea wepesi katika kila jambo la kielimu, akawahimiza waongeze juhudi katika ufuatiliaji wa masomo.

Hafla ilikua na vipengele mbalimbali vya kiutamaduni na usomaji wa mashairi pamoja na maigizo yaliyo fanywa na baadhi ya wanafunzi, yanayo lenga kuwaunganisha wanafunzi wapya na waliokuwepo.

Kumbuka kua chuo kikuu cha Al-Ameed ni taasisi ya kielimu ambayo ipo chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kinakibali cha wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu, kilianzishwa ilikiwe kitovu cha elimu kitakacho chuana na vyuo vikuu vingine vikubwa, kinatumia selebasi na mitaala ya elimu ya kimataifa inayo kiwezesha kuingia katika orodha ya vyuo bora, chuo hiki kipo katika mkoa wa Karbala barabara ya (Karbala – Najafu) karibu na nguzo namba (1238), kwa maelezo zaidi piga simu namba: (07733078000 au 07602418000) pia unaweza kutuma barua pepe kwa anuani ifuatayo: (info@alameed.iq).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: