Maktaba na daru makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu yapata maendeleo ya kisasa katika fani za elimu ya maktaba…

Maoni katika picha
Miongoni mwa harakati za maktaba na daru makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu zinazo lenga kupata maendeleo ya kisasa katika elimu za maktaba, imeshiriki katika warsha na mdahalo (workshop) iliyo fanyika kwa njia ya mtandao (webinar), warsha hii ni kwa ajili ya kubadilishana fikra na uzowefu sambamba na kutambua njia za kisasa katika elimu ya maktaba.

Miongoni mwa mada zilizo jadiliwa katika warsha hii ni: “Uendeshaji wa miradi ya kielektronik” inayo fanywa na shirikisho la maktaba za nchi za kiarabu (I’lam) kwa kushirikiana na shirika la kielektronik la (ALZAD for Digital Archiving), warsha hii inafanywa pembezoni mwa kongamano la mwaka wa ishirini na tisa wa shirikisho hilo katika mji wa Borutasudani nchini Sudani.

Chini ya anuani ya (webinar), maktaba imeshiriki midahalo kupitia intanet, muhadhiri alikua ni Profesa Clara Shoo kutoka (The “Smart” in Smarter Libraries) katika chuo kikuu cha Eneway – Ulaya. Ikashiriki pia katika mdahalo kuhusu mada isemayo: (How Does Big Data Affect You?: A Look into the Process that Drives Everyone’s Decisions) chini ya uhadhiri wa Dokta Retshard Seghal mkufunzi wa chuo cha (IGI Global) chini ya usimamizi wa taasisi ya elimu ya teknolojia katika chuo kikuu cha Arikansas Marekani.

Fahamu kua midahalo iliyo fanyika katika warsha hii ilikua inahusu njia za kisasa zaidi katika elimu ya maktaba, itakayo zifanya maktaba kua za kisasa zaidi na kutoa huduma bora kwa watafiti wa mambo mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: