Kituo cha utamaduni na habari za kimataifa Alkafeel ambacho kipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendeleza juhudi katika sekta ya elimu na utamaduni, hivi karibuni idara ya masomo na kujibu shubuha ya kituo hicho, imetoa mtiririko wa machapisho yenye anuani isemayo Athari za mazingira katika ufanyaji wa makosa na madhambi kwa lugha ya kiengereza.
Lengo la machapisho hayo, kama alivyo bainisha kiongozi wa kituo cha utamaduni na habari za kimataifa Ustadhi Jassaam Saidi kwa mtandao wa kimataifa Alkafeel kua: “Machapisho haya yanalenga kundi la vijana wa viwango tofauti na kuwaelimisha sababu za kukombolewa na Mwenyezi Mungu mtukufu kutokana na madhambi, pia kuwaelewesha athari ya madhambi kwa mwanaadamu hapa Duniani kiafya na kinafsi”.
Akaongeza kua: “Hakika kuelewesha athari za kufanya mambo ya haram ni jambo muhimu ambalo linaweza kusaidia vijana wasiyafanye, pia ujumbe wa machapisho haya haulengi vijana wa kiislamu peke yao, bali hata wasiokua waislamu, na vinaendana na mitaala ya elimu ya sasa inayo tumika, na kujibu maswali mengi anayoweza kujiuliza kila mwanaadamu wa mila yeyote ile”.
Akaendelea kusema kua: “Machapisho haya yanajuzuu (6) yameelezea mambo ya haram na makossa tofauti, yametafsiriwa na idara ya Darul Kafeel ya tarjama ambayo ipo ndani ya kituo cha utamaduni na habari za kimataifa Alkafeel, tunatarajia ndani ya muda mfupi machapisho haya yatatafsiriwa kwa lugha ya kiurdu pia”.
Tunapenda kusema kua kituo cha utamaduni na hadari za kimataifa Alkafeel ambacho kipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendelea kutoa matunda ya elimu katika sekta mbalimbali, utamaduni, utumishi, uislamu na ubinaadamu.