Kitengo cha malezi na elimu cha Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendesha semina ya kuandaa wakufunzi (TOT) kwa watumishi wa kituo cha utamaduni wa familia cha Atabatu Abbasiyya…

Maoni katika picha
Miongoni mwa harakati zake zinazo lenga kukuza mbinu za usomeshaji ikiwa ni pamoja na kuinua kiwango cha elimu kupitia kuongeza ujuzi, kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendesha semina ya kuwandaa kundi la wakufunzi (TOT), kupitia kituo cha utamaduni wa familia cha Ataba tukufu kwa muda wa siku tatu mfululizo jumla ya saa (15) za masomo.

Mkufunzi wa semina hiyo Ustadh Karraar Ma’amuury ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Warsha imepambwa na vitu mbali mbali; kuna mikanda ya audio na video inayo onyeshwa, sambamba na kuandaa mihadhara na utaratibu wa kazi na kusambaza kwa wengine, na kupima viwango vyao kupitia kazi hiyo, pia ni fursa ya kunufaika na elimu zao”.

Naye mkufunzi Ustadh Ali Shimriy ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Malengo ya semina hii ni kuandaa wakufunzi wenye uwezo wa kutambua umuhimu wa kufundisha, na kutofautisha uwelewa wa zamani na uwelewa wa sasa pamoja na kuwafanya waendane na taasisi za kielimu sambamba na kuwafanya wakidhi vigezo na sifa za mwalimu mwenye mafanikio, pamoja na kutofautisha baina ya mtazamo wa ufundishaji wa kawaida na ufundishaji wa watu wazima ikiwa kama msingi wa elimu ya usomeshaji”.

Akaongeza kua: “Kuna malengo mengine kwa mkufunzi, nayo ni namna ya kufahamu na kufanyia kazi kama msingi wa mwalimu bora, katika ufundishaji wa kitu chochote, mfundishaji huanza kazi hiyo akiwa na matarajio ya kua mwalimu mwenye mafanikio ya kweli”.

Kumbuka kua semina hii ni sehemu ya kuwafanya washiriki waendane na maendeleo ya elimu ya teknolojia pamoja na kutambua njia mpya za kisasa katika sekta ya elimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: