Kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu: vyuo vikuu vya Iraq vyafanya warsha ya kielimu kuhusu matatizo ya ubongo na maradhi ya upweke…

Maoni katika picha
Asubuhi ya Jumatano (21 Novemba 2018m) sawa na (13 Rabiul Awwal 1440h) ndani ya ukumbi wa mikutano wa chuo kikuu cha Bagdad imefanyika warsha ya kielimu kuhusu matatizo ya ubongo na maradhi ya upweke, mtoa mada alikua ni mwakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu Marekani na Afrika Kaslazini Dokta Shaamil Haadi.

Lengo la warsha hii ni kuitambulisha sekta ya elimu ya Iraq maendeleo ya kisasa yaliyo fikiwa Duniani katika tiba, muhadhara ulijikita katika kuelezea matatizo ya ubongo na namna ya kupambana nayo kwa ajili ya kuandaa kizazi chenye uwelewa mkubwa, akafafanua namna chembechembe hai zinavyo badilika katika damu na kwenye ubongo na uhusiano wake na ishara zinazo tumwa katika ubongo, akafafanua hali ya nafsi pale inapo kutana na mazingira yanayo ogopesha.

Warsha imepata mwitikio mkubwa kutoka kwa walimu na mashekhe wa Atabatu Abbasiyya na idadi kubwa ya viongozi na marais wa vitengo pamoja na walimu wa vyuo vikuu vya Iraq kutoka vitivo tofauti vya udaktari, uhandisi na vinginevyo, pia kuna wajumbe maalumu walio wakilisha baadhi ya wizara na vitengo vya serikali.

Muhadhara ulijikita katika kuelezea dalili za awali, na ulikua na athari kubwa kwa wanawarsha, kwani wamepata maarifa mapya na njia tofauti ambazo ni sehemu ya utaratibu wa warsha, mihadhara na semina bado zinaendelea kutolewa na Atabatu Abbasiyya chini ya ukufunzi wa Dokta Shaamil Haadi katika vyuo vikuu mbalimbali vya Iraq.

Washiriki wameishukuru sana Atabatu Abbasiyya kwa kuwapa nafasi ya kushiriki katika warsha hii ya kielimu, na wameonyesha utayari wao wa kushiriki katika warsha zifuatazo, pia washiriki kutoka vyuo vikuu vya Iraq wametoa shukrani nyingi kwa Atabatu Abbasiyya tukufu, kutokana na namna inavyo yapa umuhimu na kusaidia maswala ya kielimu hapa nchini kupitia vyuo vikuu.

Tunapenda kufahamisha kua Dokta Shaamil Haadi Muhsin ni msomi wa kiiraq anaeishi Marekani, alipata shahada ya Udokta (PHD) katika chuo kikuu cha Okoland huko Marekani, amefanya tafiti mbalimbali katika vituo vya kimataifa nchini Marekani, ameandika vitabu viwili ambavyo vimesambazwa katika chuo kikuu cha Mashkaan na Okoland, ameanza kutoa mihadhara na kuendesha semina tangu mwaka (2007m) katika vyuo mbalimbali vya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: