Jarida la Riyadhu Zaharaa (a.s) latangaza mashindano ya tafiti za uandishi wa habari awamu ya nne na latoa wito wa kujitokeza wanahabari wa kike…

Maoni katika picha
Miongoni mwa mikakati ya kuendeleza sekta ya habari na kuitambulisha zaidi fani ya uandishi wa habari pamoja na kuweka ushindani katika sekta ya habari zinazo husu wanawake, jarida la Riyadhu Zaharaa (a.s) linalo tolewa na ofisi ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu imetoa wito kwa waandishi na wanahabari kushiriki katika shindano la utafiti wa habari awamu ya nne, katika mada zifuatazo:

  • 1- Utambuzi wa fikra katika vita inayo endelea.
  • 2- Uwelewa wa jamii ya wanawake na vita ya vyombo vya habari vya upotoshaji.
  • 3- Nafasi ya Marjaiyya tukufu katika kutatua matatizo ya jamii za watu wa Iraq baada ya Daesh.
  • 4- Nafasi ya Marjaiyya tukufu katika kulinda haki za raia wa Iraq.
  • 5- Ulezi wa Marjaiyya kwa makundi madhaifu katika jamii za wairaq (taasisi ya Ain kama mfano).
  • 6- Nafasi ya Marjaiyya katika kulinda Dini kutokana na magenge potofu.
  • 7- Utangazaji mpya (utangazaji wa namba kwa mfano).
  • 8- Utangazaji mpya na ujao haujulikani.
  • 9- Utangazaji mpya wa sasa na maswala ya kijamii yanayo endelea.
  • 10- Utangazaji mpya na uharaka wa kusambaa uvumi.
  • 11- Picha ya mwanamke katika vyombo vya habari na changamoto ya utambulisho wake.
  • 12- Uzowefu wa wanahabari wa kike na utamaduni wa usawa.
  • 13- Uzowefu wa wanahabari wa kike na changamoto za zama.
  • 14- Kukaza roho katika mapambano ya vita ya uvumi.
  • 15- Mapambano ya wasomi katika vita ya kifikra na kubadilisha turathi na utamaduni na kuvifanya viwavutie vijana.
  • 16- Nafasi ya vyombo vya habari katika kuendeleza utamaduni na moyo ya kupambana kwa wanawake.
  • 17- Nafasi ya vyombo vya habari katika kufundisha uzalendo kwa wananchi.

Masharti ya shindano hili ni:

  • 1- Utafiti usiwe umesha wahi kuandikwa au kusambazwa.
  • 2- Usiwe chini ya kurasa (12) na wala usizidi kurasa (50) aina ya hati iwe ni (simplified Arabic) maandishi yawe ya saizi (16) na hamishi saizi (14).
  • 3- Utafiti utumwe ukiwa kwenye (cd) pamoja na nakala za karatasi sambamba na jina la mwandishi na namba ya simu na barua pepe pamoja na wasifu (cv) ya mwandishi, bila kuweka vitu hivyo utafiti hautazingatiwa.
  • 4- Uambatanishwe na muhtasari wa utafiti usiozidi maneno (300).
  • 5- Mwisho wa kupotea tafiti hizo ni (1 Rajabu 1440h).
  • 6- Utafiti uwekewa viashiria vya rejea kwa kutumia namba zitakazo wekwa bembezoni mwa maandishi (kwenye hamishi) na rejea kuandikwa mwishoni mwa utafiti.

Tafiti zitumwe kwenye anuani ifuatayo: (kitengo cha habari na utamaduni / ofisi ya wanawake / idara ya jarida la Riyadhu Zaharaa) au katika E-mail: reyadalzahra@alkafeel.net kwa maelezo zaidi piga simu namba: (07803594684).

Zawadi za washindi ni:

  • Mshindi wa kwanza: midani ya dhahabu.
  • Mshindi wa pili: midani ya fedha.
  • Mshindi wa tatu: midani ya burunzi.

Pia kuna zawadi zingine kwa washiriki, tunasisitiza kuwa utumaji wa tafiti hizo utafanyika kwa kutumia anuani ya barua pepe, na tunaomba kuzingatia hati na ukubwa wa herufi pamoja na masharti yote tuliyotaja.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: