Ugeni wa Majmaa Fiqihiyya ya Iraq ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu: Tunahitaji kuimarisha misingi ya kuishi kwa amani na kuondoa tatizo la kusambaa fikra za ubaguzi na ugaidi kwani sote tupo katika jahazi moja…

Maoni katika picha
Ugeni kutoka katika Majmaa Fiqihiyya ya Iraq ulio tembelea Atabatu Abbasiyya tukufu umesema kua: “Kipindi tulicho pitia Iraq na mambo yaliyo fanyika baada ya Daesh kuteka baadhi ya miji, inabidi tuimarishe zaidi misingi ya kuishi kwa amani na kuwe na mawasiliano ya moja kwa moja katika kuimarisha misingi hiyo, pamoja na kupambana na kusambaa fikra za ubaguzi na ugaidi kwani sote tupo ndani ya jahazi moja.

Hayo yalisemwa na rais wa ugeni huo Dokta Abdulwahabi Samaraiy ambaye aliendelea kusema kua: “Hakika inatakiwa uwepo uwelewano baina ya wanachuoni na makhatibu wa aina zote, haifai kutosheka kwa kusoma kuhusu wao na kuwajua kupitia vyombo vya habari”. Akaongeza kua: “Hakika yatupasa kuona umuhimu wa kuwa na mawasiliano ya karibu, kwani sote tupo ndani ya jahazi moja” akasisitiza kua: “Kuna ulazima wa kuheshimu utambulisho wa mtu mwingine unaye ishi naye kwa kufuata misingi ya usawa, ushirikiano na kuheshimiana, huu ndio ujumbe tunaotakiwa kuusambaza na kuusisitiza, Iraq ni sawa na ndege; hairuki kwa bawa moja, lazima iruke kwa mbawa mbili”.

Mwisho wa maongezi yake Dokta Samaraiy alionyesha furaha yake kwa kutembelea mji mtukufu wa Karbala kwa kusema: “Katika mji mtukufu wa Karbala hususan katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, tumepata furaha ya hali ya juu kwa mapokezi pora zaidi tuliyo pewa pamoja na unyenyekevu wa hali ya juu tulio uona kwa ndugu zetu maimamu na makhatibu sambamba na uwelewa wao wa hali ya juu wa misingi hii ya amani”.

Ugeni huo ulijumuisha wahadhiri wa vyuo vikuu na makhatibu wa misikiti kutoka katika mikoa ya (Bagdad, Diyala, Swalahu-Dini, Ambaar, Basra na Misaan) ulipokelewa na Shekh Ammaar Hilali rais wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, baada ya kuwakaribisha aliwaelezea mambo muhimu yanayo fanywa na Ataba tukufu katika kuendeleza elimu ya Dini na Qur’ani tukufu, pia aliwaelezea kazi zinazo fanywa na Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya kuhusu Qur’ani ikiwa ni pamoja na semina za majira ya joto (kiangazi), akawaelezea vilevile kazi ya uchapishaji wa Qur’ani tukufu, ambapo kwa mara ya kwanza Qur’ani tukufu imechapishwa katika nchi ya Iraq.

Katika mazungumzo yake pamoja na wageni aliwaambia pia majarida, semina, vitabu vya utamaduni, elimu mbalimbali na turathi vinavyo chapichwa na Ataba mbili tukufu, akamaliza mazungumzo yake kwa kusisitiza kusameheana na kujenga upendo pamoja na kufumbia macho majeraha yaliyo pita ili tuweze kuimarisha misingi ya kuishi salama kwa amani.

Mwaisho wa kikao hicho wageni waliomba salamu zao zifikishwe kwa kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, pia walipeana vitabu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: