Kuhuisha na kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume wa rehena (s.a.w.w): Atabatu Abbasiyya tukufu yaandaa mahafali ya maulidi…

Maoni katika picha
Miongoni mwa maadhimisho ya wiki ya umoja yanayo fanywa na Daru Rasuul A’adham ambayo ipo chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu katika sherehe za mazazi ya Mtume Mtukufu, asubuhi ya leo (14 Rabiul Awwal 1440h) sawa na (23 Novemba 2018m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s), imefanyika hafla ya siku ya pili na kuhudhuriwa na viomgozi wengi wa Dini na sekula pamoja na idadi kubwa ya waandishi wa habari waliokuja kuripoti tukio hili.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ikafuatiwa na ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya ulio wasilishwa na katibu mkuu Mhandsi Muhammad Ashiqar. Halafu ukafuata ujumbe wa Daru Rasuul A’adham ulio wasilishwa na rais wake Dokta Aadil Nadhiru Biriy.

Baada ya hapo akapanda mimbari mshairi Dokta Karim Mudhwahhar na kuimba kaswida iliyojaa beti za kuonyesha mapenzi na kumsifu Mtume (s.a.w.w), halafu akafuata mshairi bwana Sajjaad Abdulhadiid ambaye alimuelezea mbora wa viume (s.a.w.w) kwa beti za kaswida yake.

Hali kadhalika hafla hiyo ilipambwa na filamu iliyo onyesha harakati zinazo fanywa na Daru Rasuul A’adham, kisha vikaanza vikao vya uwasilishaji wa mada za kitafiti ambavyo viliongozwa na Dokta Daud Salmani Khalfu, zikawasilishwa mada tatu zifuatazo:

Mada ya kwanza: iliwasilishwa na Mheshimiwa Allamah Sayyid Muhammad Ali Bahrul-Uluum ikiwa na anuani isemayo: (Mtume Mtukufu na ujumbe wake kwa wote).

Mada ya pili: iliwasilishwa na Mheshimiwa Allamah Sayyid Ashukuri ikiwa na anuani isemayo: (Sababu za kufaulu kazi za Utume).

Mada ya tatu: iliwasilishwa na Dokta Numaas Almadani ikiwa na anuani isemayo: (Adabu za kuongea katika mifano ya Mtume Mtukufu, utafiti katika picha ya sinema).

Hafla ikafungwa kwa kugawa midani kwa watoa mada na washairi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: