Nukta muhimu zilizo zungumzwa na Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya Ijumaa…

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya uwanja wa haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s) leo (15 Rabiul Awwal 1440h) sawa na (23 Novemba 2018m) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Shekh Abbulmahdi Karbalai amezungumzia mambo mengi, miongoni mwa nukta muhimu alizo sema ni:

  • - Kufanya kazi na kutekeleza majukumu ni amana mbele ya Mwenyezi Mungu, kitaifa na kimaadili nao ni wajibu wa kila mtumishi.
  • - Miongoni mwa mambo muhimu katika kutekeleza majukumu ni kuhisi umuhimu wa kufanya kazi na utukufu wake kwa mtu na jamii.
  • - Ni lazima kutambua kua kufanya kazi ni jambo muhimu katika maisha yetu.
  • - Hakika Mwenyezi Mungu mtukufu amempa jukumu mwanaadamu la kua kiongozi katika ardhi.
  • - Hakika Mwenyezi Mungu mtukufu alimpa mwanaadamu amana naye akaibeba.
  • - Hakika Mwenyezi Mungu mtukufu amempa mwanaadamu jukumu la kujenga juu ya ardhi.
  • - Hakika Mwenyezi Mungu mtukufu amempa mwanaadamu jukumu la kuendeleza maisha yake.
  • - Nitakapohisi kua kufanya kazi ni jukumu nililopewa na Mwenyezi Mungu kazi hiyo itakua imepata msingi madhubuti.
  • - Muumini lazima akusudie katika nafsi yake kumridhisha Mwenyezi Mungu, na hapo ndio kazi hiyo itakua imefungamana na lengo tukufu na atapata msukumo zaidi wa kuifanya.
  • - Nitakapo jua kua kufanya jambo hili ni kutekeleza agizo la Mwenyezi Mungu na linafungamana na kumridhisha, nitalifanya kwa umaridadi na ufanisi mkubwa, jambo hili lazima lipatikane kwa mwanaadamu muumini.
  • - Inapasakua lengo linalo kusukuma kufanya kazi ni uzalendo kwa taifa na raia.
  • - Uzalendo unaweza kumfanya mtu ajitolee kufanya kazi tena kwa juhudi na didii.
  • - Wakati mwingine kupenda umashuhuri na kuhudumia watu huleta msukumo wa kazi.
  • - Unapo pungua msukumo wa kufanya kazi, ufanisi wa kazi pia hupungua.
  • - watu kuwa na malengo ya kidunia hilo ni tatizo kubwa.
  • - Miongoni mwa misingi ya imani ni kuoanisha kazi na Mwenyezi Mungu mtukufu pamoja na kutegemea radhi zake, kazi hiyo itapata mafanikio makubwa.
  • - Jamii ambayo inataasisi zinazo jikita katika kuwalea watu wapende kufanya kazi na kuiheshimu itafanikiwa.
  • - Kadri taasisi zinavyo zembea na kupunguza kuilea jamii katika utamaduni wa kupenda kufanya kazi ndio itakavyo haribika.
  • - Kadri jamii itakavyo jaa uvivu na uzembe ndio itakavyo kosa maendeleo.
  • - Nimategemeo yetu kua kila taasisi ilipe umuhimu mkubwa jambo la kufundisha kua kufanya kazi ni jambo tukufu na la heshima.
  • - Yatupasa kuwalea vizuri watoto wetu na kuwafanya waweze kutekeleza majukumu yao bila kusimamiwa.
  • - Kutunza amana ya mali na madaraka ni miongoni mwa mambo muhimu.
  • - Ili kutunza amana unatakiwa kufanya kazi na kuilinda na ufisadi na uharibifu.
  • - Kila kazi inamaadili yake lazima uyajue na kuyafuata.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: