Kazaliwa kipenzi jua linaandaza uongofu *** haiba ya mbingu juu yetu na utukufu wa kutoa.
Badru imewaangazia washirikina kwa nuru yake *** ulimwengu unanukia kwa ujio wake.
Kama kawaida yake kila mwaka katika maadhimisho ya kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari Swaadiq (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu imepambwa vizuri na imekua na mandari ya shangwe na furaha, ukumbi wa haram tukufu umepambwa vizuri na kuufanya uendane na mazingira ya maadhimisho haya makubwa kushinda yote, kwa nini isiwe hivyo wakati ni maadhimisho ya kuzaliwa kwa muokozi wa walimwengu, muongozi wa umma na kipenzi wa Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu sambamba na kuzaliwa kwa mjukuu wake Imamu Jafari bun Muhammad (a.s).
Mapambo yamewekwa katika milango yote na korido za Ataba tukufu, kwa ajili ya kuingiza furaha katika nyoyo za wapenzi na wafuasi wake watukufu, na kuwafanya waishi katika mazingira ya shangwe na furaha, yamewekwa maua kwenye milango yote ya Ataba tukufu na zimewashwa taa za rangi pamoja na kuwekwa mabango yanayo onyesha utukufu wa siku hizi.
Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalumu ya wiki hii ya Mtume inayo simamiwa na Daru Rasuul A’adham (s.a.w.w) chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu.
Tunapenda kufahamisha kua Mtume Muhammad (s.a.w.w) alizaliwa mwezi kumi na saba Rabiul Awwal mwaka wa tembo, na mjukuu wake Imamu Swaadiq (a.s) pia alizaliwa siku kama hiyo –mwezi kumi na saba- mwaka (80) hijiriyya na inasemekana mwaka wa (83) hijiriyya.