Rais wa chuo kikuu cha Al-Ameed: Chuo kikuu cha Al-Ameed kinaboresha maktaba yake kwa kuweka kila aina ya machapisho ya kielektronik yanayo endana na maendeleo ya kisasa…

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed kimepiga hatua kubwa ya kujitekemea katika ratiba zake zote za kisekula, hasa upande wa kimasomo, pia chuo kinashirikiana na jamii katika kushughulikia mahitaji ya jamii kwa kuweka ratiba ya kujitolea kwa wanafunzi na walimu sambamba na kutilia umuhimu jambo la kuendeleza uwezo wa watumishi wake katika sekta tofauti, haya yameelezwa na rais wa chuo kikuu cha Al-Ameed Dokta Jaasim Marzuuki katika ujumbe alio toa Jumapili Asubuhi (17 Rabiul Awwal 1440h) sawa na (25 Novemba 2018m) wakati wa ufunguzi wa kongamano la kimataifa la kwanza kuhusu elimu ya udaktari inayo tolewa na chuo hicho, miongoni mwa aliyo sema ni: Mwenyezi Mungu mtukufu anasema katika kitabu chake kitukufu: (Na neema za Mola wako zihadithie), tunamshukuru Mwenyezi Mungu aliye tupa neema tukufu ya elimu katika ardhi takatifu, ardhi ya shahada, kujitolea na uaminifu, kutokana na baraka za waliopo katika ardhi hii tukufu kimeanzishwa chuo kikuu cha Al-Ameed, ndani ya mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake kilikua tayali kina kila kitu kinacho husiana na masomo, kikiwa na viongozi wazuri na wanafunzi bora, sambamba na kua na vifaa vya kisasa zaidi, yote hayo yamefanikiwa kutokana na ulezi bora wa Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya Mheshimiwa kiongoza mkuu wa kisheria na katibu wake mkuu pamoja na kamati kuu ya viongozi na kamati ya malezi na elimu ya juu, na msaada usiokua na ukomo kutoa wizara ya taalimu na tarbiyya na utafiti wa kielimu katika vyuo vikuu vya kitaifa”.

Akaongeza kua: “Mwaka umeisha tangu kufunguliwa kwa chuo chetu ambacho kilifunguliwa tarehe ishirini na tisa mwezi wa kumi na moja ambayo ilisadifu siku aliyo tawazwa Imamu Mahadi (a.f), leo tunaadhimisha siku ya chuo chetu tukiwa katika sherehe za mazazi ya Mtume (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu wa sita Jafari Swaadiq (a.s)”.

Akasema: “Chuo kikuu cha Al-Ameed kimeendelea kufanya kila aina ya juhudi kuhakikisha kinafikia malengo yake ya kua chuo bora cha kupigiwa mfano katika utowaji wa elimu bora, kinacho ongoza kwa kutoa elimu nzuru pamoja na mazingira magumu inayo pitia Iraq kipindi hiki”.

Akaendelea kusema: “Chuo hakijaacha kupambana kwa ajili ya kuhakikisha kinafikia malengo yake ya kielimu, kama kinavyo jitahidi kuweka kila aina ya vifaa katika makta yake, pamoja na kuweka program za kisasa zaizi za kusomea, na kamati ya watumishi ilibidi ipewe semina elekezi na nadwa kwa ajili ya kukuza uwezo na kuwafanya waendane na maendeleo ya sasa, na kuifanya jamii iwe na vijana wanao weza kufikisha jahazi zalama.

Akamaliza kwa kusema: “Chuo kikuu cha Al-Ameed leo kinafuraha kwa kufanya kongamano hili lililo hudhuriwa na nchi sita ambazo ni: Marekani, Umoja wa falme za kiarabu, Iran, Uturuki, Lebanon pamoja na mwenyeji Iraq, jumla ya mada zilizo wasilishwa zilikua (94) zikakubaliwa mada (81) na mada (19) hazikukubaliwa, vyuo vikuu na vitivo vilivyo shiriki kwenye kongamano hili ni zaidi ya thelathini, hali kadhalika mashirika kadhaa ya kusambaza dawa yameshiriki katika kongamano hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: