Maazimio yaliyo tajwa na Marzuuki katika hafla ya kufunga kongamano lililo fanyika ndani ya ukumbi mkuu wa chuo cha Al-Ameed asubuhi ya Jumatatu (18 Rabiul Awwal 1440h) sawa na (26 Novemba 2018m) ni haya yafuatayo:
- 1- Kutegemea mkakati wa elimu uliopasishwa kwa ajili ya kufanyia tafiti za kielimu hasa katika mambo yanayo fungamana na kukidhi mahitaji ya kitaifa ya vitu vyenye uhusiano wa moja kwa moja na maisha ya raia na tafiti muhimu kielimu.
- 2- Kutegemea mkakati wa afya wa kujikomboa na tatizo la dawa mbalimbali kwa njia salama katika taasisi za afya na elimu, na kuwaelimisha watumishi wa sekta hii.
- 3- Kushajihisha kufanyika tafiti za kielimu kutokana na uwezo walio nao wa kutengeneza dawa, ili tupate dawa mpya au mbadala za thamani ndogo na uwezo mkubwa.
- 4- Kufanya tafiti za kielimu kwa ajili ya kuondoa matatizo ya kiafya yaliyopo katika sekta ya afya na kusambaza katika majaridi ya kielimu.
- 5- Kuhimiza wakufunzi na watafiti katika vyuo vikuu vya Iraq waendelee kufuatilia maendeleo ya kitabibu katika sekta tofauti kwa ajili ya kutatua matatizo sugu.
- 6- Kujikita katika tafiti za muda maalumu kwa kutumia hesabu maarufu.
- 7- Kuelekeza matumizi ya kinga na kuweka mikakati ya kufuatilia na kubalini namna ya kupambana na bakteria.
- 8- Kudumisha uhusiano baina ya vyuo vikuu na taasisi za afya za utafiti katika jamii.
- 9- Kutokana na mafanikio makubwa yaliyo patikana katika kongamano hili washiriki wanaomba liendelee kufanywa miaka ijayo.