Hospitali ya rufaa Alkafeel ya inatoa bure viungo bandia (600) kwa wanajeshi wa serikali na Hashdi Sha’abi waliopoteza viungo vyao katika vita dhidi ya magaidi…

Maoni katika picha
Haospitali ya rufaa Alkafeel inatoa bure viungo bandia (600) kutokana na kuthamiji kazi kubwa iliyo fanywa na wanajeshi wa serikali pamoja na Hashdi Sha’abi dhidi ya magaidi, katika mradi huu watashiriki madaktari bingwa kutoka India na hapa Iraq, kazi ya kufunga viungo hivyo itafanyika katika hospitali ya rufaa Alkafeel iliyopo Karbala.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Muhammad Ashiqar na balozi wa India bwana Baradim Sengo kwa kushirikiana na hospitali ya (BMVSS) Rajabuur wamezingua hema la kufungia viungo bandia lililo tengenezwa na taasisi ya kitaalamu ya Alkafeel.

Hafla ya uzinduzi wa hema hilo imehudhuriwa na mwakilishi wa wizara ya afya na mazingira Dokta Aamir Abdu Saadah, na mkuu wa idara ya afya ya Karbala Dokta Swabaah Mussawiy pamoja na rais wa kamati ya afya na mazingira ya mkoa Dokta Alaa Ghaanimiy, na jopo la viongozi wengine.

Hospitali ya rufaa Alkafeel ilikua imesha anzisha kitengo maalumu cha kufunga viungo bandia ilicho kiita Abulfadhil Abbasi (a.s), kilikua kimesha gharamia na kufunga zaidi ya viungo bandia (50) kwa wanajeshi wa serikali na Hashdi Sha’abi walioshiriki katika vita ya kukomboa ardhi ya Iraq kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh, baada ya kuingia mkataba na shirika moja la Swiden.

Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zinazo tolewa na hospitali ya rufaa Alkafeel unaweza kutembelea toghuti ya hospitali ambayo ni: www.kh.iq au piga simu namba: (07602344444 / 07602329999).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: