Idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu inayo ongozwa na kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) kikosi cha 26/ cha Hashdi Sha’abi, kwa kushirikiana na ofisi ya ustawi wa jamii ya mkoa wa Baabil na Swalahu Dini, imegawa misaada ya kibinaadamu kwa wakazi wa maeneo yaliyo pata mafuriko kutokana na mvua kubwa zilizo nyesha katika mkoa wa Swalahu Dini kwenye vijiji viwili (Huriyya na Khadharaniyya).
Misaada hii imetolewa katika oprosheni ya (kutumikia taifa) inayo fanywa na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapihanaji, kwa maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa viongozi wa ustawi wa jamii walio elekeza kwenda kusaidia wakazi wa Sharqaat na miji mingine.
Kumbuka kua uongozi wa kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s), kimejiandaa kutoa misaada ya kibinaadamu katika mikoa yote, kimeunda kamati ya kutoa misaada ya haraka kwa waathirika wa mafuriko katika mikoa iliyo pata mvua nyingi siku chache zilizo pita.
Viongozi wa kikosi wamejipanga vizuri na wameita kikosi kimoja cha hakiba kuja kushiriki katika kazi ya kutoa misaada na kuandaa mahitaji ya dharura.
Miji mingi hapa Iraq ilipata mvua nyingi siku chache zilizo pita ikiwa ni pamoja na mkoa wa Nainawa, Swalahu Dini, Karkuuk na Waasit.
Tunapenda kukumbusha kua; kazi ya kwanza iliyo fanywa na kamati ya ustawi wa jamii ya Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya usimamizi wa kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) ya kutoa misaada katika mikoa (12) aliyo athirika na mafuriko, ilifanyika asubuhi ya Jumatano (17 Muharam 1440h) sawa na (27 Septemba 2018m).