Atabatu Abbasiyya tukufu inajiandaa kushiriki maonyesho hayo chini ya kaulimbiu isemayo: (Miradi yetu inachochea kujitegemea kwa Iraq) pamoja na kwamba inasaidia viwanda vya ndani na uzalishaji wa Iraq, maonyesho haya yatatoa fursa ya kuonyesha bidhaa zinazo tengenezwa na Atabatu Abbasiyya kwa mikono ya wananchi wa Iraq, ambazo zinanafasi kubwa katika kukuza sekta ya viwanda, kilimo na uchumi wa taifa.
Atabatu tukufu katika maonyesho haya itawakilishwa na:
- 1- Kundi la vitalu vya Alkafeel: wataonyesha vitu wanavyo zalisha katika vitalu pamoja na asali.
- 2- Shirika la Nurul Kafeel: linalo tengeneza bidhaa za wanyama: litaonyesha aina mbalimbali za vyakula vya wanyama wanavyo tengeneza.
- 3- Shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud: litaonyesha bidhaa linazo tengeneza, ikiwa ni pamoja na; visafishio, kinga, dawa za kuondoa chunvi asilia na namna ya kupambana na magonjwa mbalimbali ya mimea.
- 4- Shirika la ujenzi viwanda na biashara, Liwaaul Aalamiyya: litaonyesha bidhaa linazo tengeneza, ikiwa ni pamoja na vifaa vya ujenzi (matofali na nguzo) za ukubwa na aina mbalimbali.
- 5- Darul Kafeel ya uchapishaji na usambazaji: itaonyesha machapisho yake na vifaa wanavyo tumia.
- 6- Shirika la uchumi Alkafeel ambalo lipo chini ya kitengo cha kilimo na wanyama: litaonyesha mazao yanayo limwa katika mashamba ya Khairaat Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na kuonyesha filamu za mashamba darasa na mashamba ya Anwaaru Saaqi, mashamba ya Qaadhwi Haajaat.
- 7- Shirika la ulinzi na mawasiliano Alkafeel: litaonyesha huduma linazo toa na njia za mawasiliano na mengineyo.
Tunapenda kujulisha kua maonyesho haya yanasimamiwa na wizara ya biashara kupitia mashirika mbalimbali ya biashara, kwa kushirikiana na wizara ya viwanda na madini pamoja na umoja wa viwanda vya Iraq.