Kamati ya maandalizi ya kongamano la kimataifa kuhusu elimu za lugha ya kiarabu yatangaza mada zitakazo shindaniwa na yatoa wito kwa watafiti wajitokeze kushiriki katika shindano hilo…

Maoni katika picha
Katika kukamilisha mfululizo wa vikao vyake vya kuandaa kongamalo liitwalo: (Hauza ni kitovu cha mabadiliko) ambalo hufanywa kwa ushirikiano baina ya Atabatu Abbasiyya na taasisi ya Bahrul-Uluum Alkhairiyya, kamati ya maandalizi imetangaza kufanyika kwa kongamano la awamu ya nne lenye anuani isemayo: (Kongamano la kimataifa awamu ya nne kuhusu elimu za kiarabu na fani zake baina ya changamoto na mabadiliko) litakalo fanyika tarehe (14 – 15 Machi 2019m) na kuwataka watafiti na wasomi waangalie kwa makini kanuni za lugha ya kiarabu, na kufichua hazina kubwa iliyopo katika lugha hiyo upande wa mazingira, utamaduni, jamii na siasa…

Na nafasi yake katika kuhuisha elimu za kiarabu na fani zake, kupitia mada zifuatazo:

Mada ya kwanza: Hauza na elimu za kiarabu na fani zake, uandishi, usambazaji na uhakiki.

Mada ya pili: Hauza na kuhuisha lugha ya kiarabu na fani zake pamoja na kuifundisha kwa wasiokua waarabu.

Mada ya tatu: Hauza na fani za kiarabu.

Mada ya nne: Hauza na usomaji wa dalili za kidini.

Mada ya tano: Hauza na hali halisi ya lugha ya kiarabu ya sasa na baadae.

Masharti ya kuandika tafiti hizo ni:

  • - Utafiti usiwe umeshawahi kuandikwa au kutolewa na wengine kabla yako.
  • - Utafiti uzingatie vielelezo halisi sio vya kufikirika.
  • - Utafiti uendane na mada tulizo toa.
  • - Ufuate misingi na kanuni za kielimu katika uandishi.
  • - Kamati hailazimiki kurudisha utafiti kwa mwandishi wake.
  • - Tafiti zote zitachujwa na kamati maalumu ya majaji.
  • - Tafiti ziwasilishwe zikiwa zimechapishwa katika karatasi za (A4) huku naka moja ikiwa imehifadhiwa kwenye (CD) na iandikwe kupitia program ya (word) na isizidi kurasa ishirini na tano kwa hati ya (Simplified Arabic) na herufi zenye ukubwa wa saizi (16).
  • - Mwandishi aambatanishe na muhtasari wa utafiti wake pamoja na wasifu wake (cv) na namba ya simu sambamba na anuani yake ya barua pepe.
  • - Mwisho wa kupokea tafiti hizo ni (1/2/2019m).

Unaweza kuwasiliana na kamati ya maandalizi kupitia njia zifuatazo:

Simu namba: (009647802222543).

Parua pepe: info@h-najaf.iq

Toghuti: www.h-najaf.iq

Facebook: https://www.facebook.com/hawza.najaf

Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: