Imamu Swadiq (a.s) alimuambia ammi yake Abbasi (a.s) katika ziara maarufu aliyo wafundisha wafuasi wake kua: ((Amani iwe juu yako ewe mja mwema, mtiifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kwa waumini na kwa Hassan na Hussein (s.a.w.w)).
Hakika utiifu wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kaka yake Imamu Hassan Zakiy unaonyesha nafasi aliyo nayo kwake, wala sio nafasi ya kawaida, bali ni nafasi kubwa na tukufu mno, kwani alikua anamtii akielewa wazi na akiwa na imani madhubuti, kwani (a.s) alikua anaonekana akimtii sawa na kumtii baba yake kiongozi wa waumini (a.s), aliwahusia watoto wake na watu wote wa nyumbani kwake, na wafuasi wake pamoja na wapenzi wao (a.s) kumsikiliza na kumtiii Imamu Hassan Almujtaba (a.s), kisha baada yake Imamu Hussein (a.s).
Miongoni mwa mambo yanayo onyesha pia utukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kaka yake Imamu Almujtaba (a.s), ni pale alipo shirikishwa na Imamu Hussein (a.s) katika kumuosha Imamu Almjtaba (a.s) na kumvisha sanda, pamoja na kwamba Maasumu anapo kufa haandaliwi ispokua na mtu ambaye ni Maasumu kama yeye.
Ni wazi kua: Abulfadhil Abbasi (a.s) kushirikishwa katika kumuandaa kaka yake Imamu Almujtaba (a.s), kunatokana na usia wake kwa mdogo wake Imamu Hussein kua amshirikishe katika kumuandaa, na Imamu Hussein (a.s) pia akaona utukufu wake ndio akamshirikisha katika kuandaa mwili wa kaka yao, kama kiongozi wa waumini alivyo mshirikisha mtoto wa ammi yake Fadhili bun Abbasi bun Abdulmutwalib katika kumuandaa Mtume (s.a.w.w), lakini alimuambia afumbe macho yake, kwa kuogopa asipofuke iwamo jicho lake likiuona mwali mtakatifu wa Mtume (s.a.w.w), Fadhili sio maasumu na haifai kwa asiye kua maasumu kuangalia mwili wa maasumu anapo andaliwa, na iwapo akiangalia macho yake yanapofuka.
Lakini Abulfadhil Abbasi (a.s) alishirikiana na kaka yake Imamu Hussein (a.s) katika kumuonsha Imamu Almujtaba (a.s), wala hakuna ushahidi wa kihistoria kua alifumba macho yake wakati wa kumuosha kaka yake, jambo hili linaonyesha ukubwa wa heshima ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na utukufu wake.