kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) chakumbuka ushujaa wa mashahidi wake…

Maoni katika picha
kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) kimefanya hafla ya kuwakumbuka mashujaa wake waliouwawa wakiwa katika kazi ya kulinda taifa hili tukufu, hafla hiyo imefanyika kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, katika mnasaba wa kumbukumbu ya nne ya jahazi la mashahidi wa vita ya ukombozi, ambao ni shahidi Kamanda Wasaam Sharifu na kamanda Maliki Yahaya, na shahidi Aqiil Jaabir na Qassim Khalf. Hafla hiyo ilikua na kauli mbiu isemayo: (kwa shahidi), imehudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar pamoja na viongozi wengi wa askari wa Karbala na viongozi wa serikali ya mkoa, imehudhuriwa pia na wawakilishi wa kikosi cha Furat Ausat na wawakilishi wa Hashdi Sha’abi sambamba na idadi kubwa ya wapiganaji wa fatwa ya kujilinda na familia za mashahidi pamoja na mazuwaru.

Baada ya kusoma Qur’ani ya ufunguzi kisha kusimama na kusoma surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi watukufu wa Iraq na kusikiliza wimbo wa taifa, ulifuata ujumbe wa kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi Ustadh Maitham Zaidiy, miongoni mwa aliyo sema ni: “Tumekutana kuwakumbuka watu watukufu waliojitolea nafsi zao kwa ajili ya taifa hili, kufuatia kuitikia kwao wito wa Marjaiyya na wito wa taifa lilipo vamiwa na magaidi wa Daesh, wakazima njama za maadui na kuwaangamiza”.

Akaongeza kua: “Leo tunakumbuka makamanda ambao walitutoka katika mwaka wa kwanza wa vita takatifu ya jihadi ya kujilinda walio uwawa katika wilaya ya Balad na Dujail, zilizokua zimetekwa na magaidi wa Daesh, kikosi cha cha wapiganaji kilielekea katika wilaya hizo kwa maelekezo ya uongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu Ili kwenda kuwakomboa wakazi wa wilaya hizo kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh, mazingira ya vita yalikua magumu sana, zilikua zinahitajika deraya za kivita, wapiganaji walisonga mbele wakiongozwa na kamanda Sayyid Wasaam na Sayyid Maliki, wakafanikiwa kukomboa eneo kubwa katika vita hiyo ambayo waliuwawa”.

Akasisitiza kua: “Tunawaahidi mashahidi wetu kua bado tunafuata njia ya jihadi na kulinda taifa hili pamoja na maeneo matukufu tunakamilisha harakati zao tukufu, na tunasimama kwa heshima kubwa pamoja na familia zao zilizo jitolea wapenzi wao kwa ajili yetu, tunazishukuru pia Ataba tukufu zilizo toa kila aina ya misaada kwa vikosi vya wapiganaji wa Hashdi Sha’abi na wanajeshi wa serikali, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tutakamilisha safari hii, vilevile tunaishukuru serikali ya mkoa wa Karbala iliyo tangaza kuanzishwa kikosi cha wapiganaji na kukisaidia, hali kadhalika tunakishukuru kikosi cha Furat Ausat”.

Katika hafla hiyo ilionyeshwa filamu fupi ya vita waliyopigana makamanda hao, pamoja na kusomwa mashairi mbalimbali yaliyo onyesha mapenzi na uzalendo wa taifa la Iraq, kutoka kwa mshairi Najaah Arsaan na Muhammad A’ajibiy pamoja na mshairi na mwimbaji Thaamir A’aridhiy.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: