Vipengele muhimu vilivyo ongelewa na Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa…

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya uwanja wa haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s) leo (22 Rabiul Awwal 1440h) sawa na (30 Novemba 2018m) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, amezungumzia vipengele kadhaa vya kimaadili na kimalezi vinavyo endana na mazingira tunayo ishi, miongoni mwa aliyo sema ni:

  • - Katika kila jamii kuna matatizo, baadhi ya matatizo hutokea kwa sababu ndogondogo tena za kipuuzi.
  • - Taratibu za kimazingira na sheria za Mwenyezi Mungu zimeweka mipaka, na kutaka isivunjwe, mtu anapoivunja hutakiwa aadhibiwe.
  • - Mwenyezi Mungu mtukufu ametupa mzani wa kupimia vitendo vyetu, kabla ya kutuletea sheria yake tukufu nao ni akili.
  • - Kila mtu kwa kutumia akili yake anaweza kufahamu kua hili linafaa kufanywa au halifai.
  • - Mtu hufanya mabaya huku anajua kama ni mabaya.
  • - Mtu mwenye akili ndio tajiri.
  • - Kwa kutumia akili mtu hutambua nini chakufanya.
  • - Miongoni mwa faida za akili humsaidia mwanaadamu kufahamu mambo nayo ni neema kubwa.
  • - (Adui mwenye akili ni bora kuliko rafiki mjinga) kwa sababu adui mwenye akili utajua namna ya kuamiliana nae.
  • - Akili inamisingi yake wakati ujinga hauna misingi.
  • - Ufakiri sio jambo la aibu na wala sio kikwazo lakini mtu anapokua mjinga atakua fakiri.
  • - Mjinga anayejiona mwerevu hawezi kusoma, kwa sababu anajiona anajua na huo ni ujinga mara mbili (jaahilu murakkabu) hiyo ni hatua mbaya zaidi ya ujinga.
  • - Mtu mwenye akili unaweza kujadiliana naye.
  • - Ujinga mara mbili (jaahilu murakkabu) ni tatizo kubwa.
  • - Mjinga mara mbili ni mtu asiyejua na hajui kama hajui.
  • - Mtu mwenye akili anauwezo mkubwa wa kufanikiwa.
  • - Umma mzima uliangamia kwa sababu ya ujinga.
  • - Ujinga ni kazi kuumaliza ispokua kwa kusoma na watu kuhisi umuhimu wa kutumia akili kwani akili ndio nyenzo ya kutafutia elimu.
  • - Ujinga ni upotofu na kutokua na maarifa.
  • - Mtu hurithishwa adabu nayo hufanya aheshimiwe, huambiwa huyu anaelimu na adabu.
  • - Mlango wa maadili, kusoma, uwelewa yote msingi wake ni Adabu.
  • - Hekima namba 58 katika kitabu cha Nahjul Balagha ya sharifu Ridhwa inasema: (Atakae omba ushauri kwa watu atakua amezishirikisha akili zao).
  • - Wanachuoni wengi na waja wema walikua hawalali na jambo bila kuomba ushauri kwa watalamu wa jambo hilo, na kuufanyia kazi ushauri mzuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: