Miongoni mwa orodha za turathi teule: kituo cha turathi za Karbala chatoa kitabu kwa jina la: (Shekh Muhammad Taqii Shirazi Alhaairiy na nafasi yake kisiasa katika miaka ya 1918 – 1920m).

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Karbala ambacho kipo chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimekua kikitoa mtiririko wa machapisho ya turathi chini ya utaratibu walio jiwekea, kufuatia utaratibu wa turathi teule hivi karibuni kimetoa kitabu kwa jina la: (Shekh Muhammad Taqii Shirazi Alhaairiy na nafasi yake kisiasa katika miaka ya 1918 – 1920m). ambacho kimeandikwa na Dokta Alaa Swafi.

Kitabu hiki ni sehemu ya muendelezo wa kazi ya uandishi na uhakiki wa turathi zetu, kina sehemu tatu,historia ya maisha ya Shekh Muhammad Taqii Shirazi (mmoja wa Marjaa maarufu wa kishia, na mmoja wa wapambanaji wa harakati ya ishirini dhidi ya uvamizi wa Uingereza hapa Iraq) na nafasi yake katika uwanja wa siasa za Iraq, ndani ya miaka hiyo miwili ambayo ilijaa matukuo mengi yaliyo likumba taifa hili, miongoni mwa matukio hayo ni mapambano ya watu wa Iraq dhidi ya uvamizi wa Mwingereza.

Kumbuka kua kitabu hiki kinaonyesha namna kituo cha turathi za Karbala kinavyo jali urithi wa wanachuoni wa mji wa Karbala na kazi walizo fanya, pia ni mwendelezo wa kazi nyingi zinazo fanywa na kituo za kuandika na kuhakiki turathi mbalimbali za mji mtukufu wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: